Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siyo tu kukuongezea maarifa, kujielimisha ni sehemu ya burudani muhimu katika mwili. Katika maandiko na filamu vipo vitu vinavyofanana na maisha halisi ambavyo husaidia kutoa suluhu ya kuvishughulikia.



Kuwa tayari kwa lolote

Binadamu anapanga lakini siyo mwamuzi wa mwisho. Mpangaji mkuu ni Mwenyezi Mungu. Hivyo lolote linaweza kutokea kabla ndoto haijawa halisi kwa maana hiyo ni vizuri kuwa tayari.
 
Pia, unaweza kupata maradhi, kufiwa na ndugu wa karibu au majanga ya mafuriko au moto yatakayoteketeza kila ulichokiwekeza kwa miaka kadhaa.

Kwa majanga ambayo unaweza kuyawekea kinga kama vile kukatia bima ni vyema ukafanya hivyo ili kupunguza makali pale yatakapotokea.

Kata bima ya nyumba, gari na maisha. Weka vifaa vya kukabiliana na moto nyumbani kwako au ofisini na ujifunze kuvitumia.
 
Unapoteleza juu ya ganda la ndizi na kudondoka, akilini mwako kitakachokuja kwa haraka ni kujiuliza nani amekula ndizi na kutupa ganda kiholela. Ukweli ni kwamba kama ungekuwa makini unapotembea kwa kutazama chini, ungeliona na kulikwepa.

Unaposhindwa jambo usitafute sababu ya kujitoa badala yake tafuta njia mbadala ya kuhakikisha kazi hiyo inafanikiwa.
 
 Je, unataka kuacha kuvuta sigara? Sawa, nakubaliana na wewe lakini unajua kwa nini unataka kuacha tabia hiyo ambayo umeizoea kwa muda mrefu?. Kwa sababu haitoshi tu utake kuacha kuvuta sigara bila kuwa na sababu muhimu inayokusukuma uache suala hilo. Kwa hivyo kwanza anza kujiuliza kwa nini unataka kuacha sigara. Kujua sababu kutakusaidia katika kutekeleza lengo lako vyema.
 
Je, unaacha sigara kwa kuwa unataka kuilinda familia yako isipate madhara ya sigara unazovuta? Je, unataka kuacha sigara kwa kuwa umeogopa kupata kensa ya kifua? Au je, ungependa kuonekana kijana zaidi? Tafuta sababu muhimu ambayo itaizidi hamu yako ya kuvuta sigara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…