Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Jua kuwa ni jambo gumu kuacha tabia uliyoizoea kwa muda mrefu mara moja. Haitowezekana utupe kipande chako cha sigara yako mara moja na kutangaza kuwa umeacha kuvuta. Suala hilo ni gumu kwani asilimia 95 ya watu wanaojaribu kuacha sigara kwa mtindo huo hushindwa, inabidi upate ushauri na tiba mbadala ili kukusaidia kuacha kuvuta sigara, hii ni kwa sababu sigara inaleta uraibu wa nicotine, na ubongo unaizoea mada hiyo hivyo kuacha kuvuta husababisha uhisi dalili za kukosekana nicotine katika ubongo.