Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kifungua kinywa hiki pia kinawawezesha wanafunzi kufaulu vizuri mitihani yao na kupata alama za juu kwa mitihani waliyofanya kabla ya mapumziko yao ya mchana…nguvu hizo zinazotokana na kifungua kinywa cha uji wa ulezi zimeimarisha kiwango chao cha sukari kwenye ubongo, na zimeimarisha uwezo wa kufikiri, pia kuwa wasikivu.” alisema.
 
Pia alisema kuwa ndani ya uji wa ulezi kuna virutubisho muhimu vya kuifanya akili kufanya kazi ya kuwa na kumbukumbu na mwili kuwa na nguvu kubwa katika kumfanya mtoto awe na ari ya kujisomea ndio maana hata mama wajawazito wanashauriwa kunywa uji wa ulezi mara baada ya kujifungua ili kurudisha nguvu.
 
Wakati wa miaka 70 tulikuwa tunashindia uji wa ulezi kutokana na virutubisho vilivyomo ndani yake kwa kuwa vilitupatia nguvu kubwa ya kuufanya mwili kuwa na nguvu ya ziada kwa muda mrefu , lakini kwa kuwa sasa hivi watoto wetu wengi hawapewi uji wa ulezi asubuhi hivyo hawawezi kuwa na uvumilivu wa kushinda muda mrefu bila kula” alisema.
 
Kwa kuunga mkono hoja hizo naye Dk. Raymond Shirikisho kutoka KCMC alisema kuwa mwili wa binadamu unafanya kazi kama mashine hivyo kama kuna kifaa hakina mafuta muhimu na ya kutosha basi si rahisi msuguano kutokea ili mashine ifanye kazi, hivyo unywaji wa kifungua kinywa asubuhi na mapema unapoamka ni muhimu kwa afya ya akili.
 
Walitoa wito kwa jamii kurudi katika kula vyakula vya asili na kuachana na vyakula visivyo na tija katika mwili wa binadamu. “Wazazi wanaaswa kuwandalia watoto wao uji wa ulezi asubuhi na mapema kabla hawajatoka kwenda shuleni ili kuweza kufungua akili ya mtoto na kuwajengea uwezo mkubwa wa kufikiri,”alisema Nyampiga.
 
Miongoni mwa viungo maarufu sana na vinavyopendwa na watu wengi kutumika katika matumizi ya vyakula ni pili pili manga, kiungo hiki hutumiwa na watu wengi kwa kujua ama kutokujua kawa ina faida nyingi kiafya katika kuboresha afya ya mwili. Pilipili manga hujulikana sana hasa na watu wa jamii za pwani kwa kuwa asili yake ni kutoka katika bara la Asia hivyo ilianza kutumika baada ya wakoloni kutoka asia walipodhuru maeneo haya ya nchini.
 
Hujulikana kwa jina la kingereza kama Sichuan pepper na kwa jina la kisayansi kama Zanthoxylum,wengi hupenda kuitumia katika kupikia pilau ama kuweka katika uji. Tafiti mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zimelezea kuwa pilipili manga hutibu na kukinga magonjwa mbalimbali mwilini, baadhi ya mgonjwa hayo ni pamoja na presha, nuru ya macho, huzuia saratani, huongeza hamu ya kula, huongeza hamu ya tendo la ndoa,
 
huzibua mirija ya uzazi, huongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha na pia huondoa maumivu ya kifua. Pia huimarisha mzunguko wa damu mwilini, huongeza kinga ya mwili, huimarisha mifupa, kuongeza joto mwilini, na kutibu bawasiri. Dk. Diana Bautista mtalaamu wa masuala ya akili kutoka chuo kikuu cha Califonia aliwahi kusema kuwa miongoni mwa viungo
 
anavyostajabishwa navyo katika kuweka sawa kumbu kumbu ni pamoja na matumizi ya pili pili manga. “Nilishikwa na mshangao baada kutembelea moja ya maabara na kugundua kuwa baadhi ya vileta hisia (Receptors) mwilini vilivyokuwa vimelala kwa kutokufanya kazi lakini baada ya wagonjwa hawa kutumia kiungo hiki viungo hivi viliamka na kuanza kufanya kazi” alisema Dk.
 
Bautista. Pia aliongezea kwa kusema kuwa mfumo wa fahamu mwilini unahamasishwa katika kufanya kazi zaidi pale unapotumia kiungo hiki cha pili pili manga. Naye Dk. Raphael Nyampiga kutoka kliniki ya Atukuzwe iliyoko Pugu jijini Dar es salaam aliliambia gazeti hili kuwa kiungo hiki ni maarufu sana hasa kwa jamii ya watu wa Asia kwa kuwa wanafahamu umuhimu wake katika kuweka sawa mfumo wa fahamu hasa kwa wale wazee sana ambao wanaelekea kupoteza kumbukumbu na kwa wale walio pooza ni muhimu kutumia kiungo hiki.
 
NAye Dk. Zawadi Abdallah kutoka zawadi herbalist anaongezea kwa kusema kuwa pilipili manga huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa jinsia zote kwa mwanamke na kwa mwanaume kwa kuwa mfumo wa fahamu mwilini unafanya kazi vizuri . Pia aliendelea kufafanua kwa kusema kuwa matumizi ya kiungo hiki cha pili pili manga huzibua mirija ya uzazi kwa wanawake na kwa wanaume kwa kuondoa visababishi vya mirija kuziba katika mwili na kusafisha mirija.
 
Screenshot_2017-08-11-17-48-50.png
[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22]
 
Bautista. Pia aliongezea kwa kusema kuwa mfumo wa fahamu mwilini unahamasishwa katika kufanya kazi zaidi pale unapotumia kiungo hiki cha pili pili manga. Naye Dk. Raphael Nyampiga kutoka kliniki ya Atukuzwe iliyoko Pugu jijini Dar es salaam aliliambia gazeti hili kuwa kiungo hiki ni maarufu sana hasa kwa jamii ya watu wa Asia kwa kuwa wanafahamu umuhimu wake katika kuweka sawa mfumo wa fahamu hasa kwa wale wazee sana ambao wanaelekea kupoteza kumbukumbu na kwa wale walio pooza ni muhimu kutumia kiungo hiki.
 
Back
Top Bottom