Kuegesha gari mbali na nyumbani ili wakati unatoka utembee kidogo kufuata gari. Kitu kingine unachoweza kufanya kwa wakati huu ni kujitahidi kutembea bila kutumia usafiri binafsi ili kuufanya mwili utoke jasho ambalo litakusaidia kupunguza uzito huku ukiwa na furaha yako kama kawaida.
Mbali na hilo unaweza pia kuruka kamba, au kufanya usafi wa kwenye bustani pembeni ya nyumba kama kuna nafasi kabla ya kuanza pilikapilika nyingine na hii pia aihitaji muda mwingi dakika 10 zinatosha.
Hakuna haja ya kutumia fedha nyingi wakati huu kwa ajili ya kwenda gym, unaweza kufanya mazoezi kwa njia ya simu. Kuna simu ambazo zina tipu za mazoezi ni muhimu kuzifuata hizo kwa dakika 30 kulingana na unachokitaka.
Mazoezi haya ya kwenye simu ni bure na ukifungua utapata vitu vingi ambavyo vitakusaidia kuifanya sikukuu yako iwe ya furaha huku ukiuweka mwili wako fiti.
Aina za mazoezi unazoweza kufanya kwa kipindi hiki
Kukimbia Polepole:Kwa mujibu wa Lawrence J. Cheskin, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa kituo cha Johns Hopkins Weight Management, anasema kuwa kukimbia polepole ndiyo njia bora zaidi ya kuwa na moyo wenye afya.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.