Hata mtoto huwezi pata bila maji!Kwa uchache, binadamu anatakiwa kunywa maji yasiyopungua glasi nane kila siku. Kiwango hicho kitaongezeka iwapo mtu ana uzito mkubwa na shughuli zake nyingi zinatumia maji mengi mwilini. Hivyo kiasi hicho cha glasi nane ni kiwango cha chini kabisa anachotakiwa kunywa mtu hata kama hana kazi yoyote.