Ndiyo maana hata Mwl alishindwa. Kuna watu aliamini kuwa walikuwa wafuasi wa nadharia zake na walikuwa waadilifu kama yeye, wengine akazunguka mpaka nchi nzima kuwapigia kampeni za urais, kumbe walikuwa ni majibwa katika ngozi ya kondoo. Ni tatizo la mfumo na falsafa ya jamii. Ni vigumu sana kuwa na kiongozi mwadilifu kwenye jamii inayoabudu mafisadi na majizi makubwa makubwa. Ukipewa cheo ukawa mwadilifu sana ukija kuondoka hujatajirika jamii inakucheka. Ukiiba na kujenga majumba 70 kama akina Masamaki basi we ndo mjanja na mwanaume wa shoka. Kama akina Joka Makengeza ndiyo vioo vya jamii unategemea nini?