Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati huohuo mifupa mipya inayotokeza huanza kukua karibu na kiungo. Uvimbe unaweza kutokea, na mfupa ulio chini ya gegedu huwa mzito na kuharibika umbo. Dalili nyingine za ugonjwa huo ni, vinundu kwenye viungo vya vidole, sauti ya kusugua katika viungo vilivyoathiriwa, mishtuko ya ghafula ya misuli, na vilevile maumivu, kukakamaa, na kushindwa kusogeza viungo.
 
Zamani, ilidhaniwa kwamba ugonjwa huo ulitokea tu kwa sababu ya uzee. Hata hivyo, wataalamu wametupilia mbali dhana hiyo ya kale. Jarida la The American Journal of Medicine lasema hivi: “Hakuna uthibitisho wowote kwamba kiungo cha kawaida kinachofanya kazi ya kawaida tu kitaharibika katika kipindi cha maisha.” Basi, kisababishi cha ugonjwa huo wa osteoarthritis ni nini? Gazeti la Uingereza la The Lancet linasema kwamba jitihada za kuelewa kisababishi cha ugonjwa huo “zimetokeza ubishi mwingi.”
 
Baadhi ya wachunguzi wanafikiri kwamba huenda mfupa ulikuwa umejeruhiwa mbeleni bila kugunduliwa. Halafu, huenda madhara hayo yakasababisha ule ukuzi wa mfupa unaotokeza na vilevile kuharibika kwa gegedu. Wengine wanadhani kwamba ugonjwa huo huanzia katika gegedu yenyewe. Wanafikiri kwamba gegedu hiyo inapoharibika na kuchakaa, shinikizo kwenye mfupa unaokinzwa na gegedu hiyo huzidi. Mabadiliko katika viungo hutokea mwili unapojaribu kutengeneza gegedu iliyoharibika.
 
Ni nani hasa anayeweza kupata ugonjwa huo? Ijapokuwa si uzee unaosababisha ugonjwa huo, uharibifu wa gegedu huwaathiri hasa wazee. Wengine wanaoweza kupata ugonjwa huo ni watu ambao wana kasoro fulani katika viungo vyao, au wale wenye misuli dhaifu ya miguu na mapaja, miguu isiyo na urefu sawa, au kasoro katika uti wa mgongo. Kiungo kilichojeruhiwa katika aksidenti, au kutumia kiungo fulani kupita kiasi kazini kunaweza pia kusababisha ugonjwa huo. Baada ya uharibifu wa gegedu kuanza, kunenepa kupita kiasi kunaweza kuuzidisha.
 
Dakt. Tim Spector anasema hivi: “Osteoarthritis ni ugonjwa tata ambao mara nyingi husababishwa na hali ya mazingira tunamoishi lakini hurithiwa vilevile.” Hasa wanawake wa makamo na wanawake wazee walio na watu wa ukoo wenye ugonjwa huo wanakabili hatari ya kuupata. Ni watu walio na mifupa migumu hasa wanaopata ugonjwa wa osteoarthritis, tofauti na ugonjwa wa osteoporosis unaodhoofisha mifupa. Watafiti fulani wanasema pia kwamba madhara yanayosababishwa na molekuli ya oksijeni yenye idadi ya elektroni isiyogawanyika kwa mbili, na upungufu wa vitamini C na D, unaweza kusababisha ugonjwa huo.
 
Matibabu

Matibabu ya yabisi-kavu kwa kawaida huhusisha kutumia dawa, mazoezi ya mwili, na kubadili namna ya kuishi. Huenda tabibu wa maungo akaanzisha matibabu ya mazoezi ya mwili. Mazoezi hayo yanaweza kuhusisha mazoezi ya kukaza misuli, mazoezi yanayoboresha mfumo wa kupumua na mzunguko wa damu, kama vile kutembea au kukimbia, na mazoezi ya misuli ya kuinua vitu vizito. Mazoezi hayo yamesaidia sana kupunguza dalili nyingi kama vile uvimbe na maumivu ya viungo, unyong’onyevu, uchovu, na kushuka moyo.
 
Mazoezi hayo hunufaisha hata wale walio wazee sana. Mazoezi yanaweza pia kuzuia kudhoofika kwa mifupa. Watu fulani wanadai kwamba maumivu yanaweza kupunguzwa kwa matibabu mbalimbali ya maungo kwa kutumia joto na baridi na kwa tiba ya vitobo.*

Kupunguza unene kunaweza kusaidia sana kutuliza maumivu ya viungo yanayosababishwa na yabisi-kavu. Inasemekana kwamba chakula kinachoweza kupunguza unene na vilevile maumivu ni chakula chenye kalisi nyingi kama vile mboga, matunda, na samaki wanaoishi katika bahari zenye maji baridi sana wenye asidi-mafuta nyingi inayoitwa omega-3.
 
Chakula kilichotayarishwa katika viwanda na chakula chenye mafuta yenye asidi nyingi kiepukwe. Vyakula hivyo maalumu vinasaidia vipi? Inasemekana kwamba vyakula hivyo huzuia uvimbe. Wengine wanasema kwamba wamesaidiwa kwa kutokula nyama, vyakula vinavyotengenezwa kwa maziwa, ngano, na jamii ya mboga za mtunguja, nyanya, viazi, pilipili, na biringani.

Baadhi ya wagonjwa wanapendekezewa upasuaji unaohusisha kuingiza chombo fulani ndani ya kiungo chenyewe, na kuondoa utando unaotokeza vimeng’enya vinavyoharibu gegedu. Hata hivyo, mara nyingi uvimbe hurudi baada ya upasuaji huo.
 
Chakula kilichotayarishwa katika viwanda na chakula chenye mafuta yenye asidi nyingi kiepukwe. Vyakula hivyo maalumu vinasaidia vipi? Inasemekana kwamba vyakula hivyo huzuia uvimbe. Wengine wanasema kwamba wamesaidiwa kwa kutokula nyama, vyakula vinavyotengenezwa kwa maziwa, ngano, na jamii ya mboga za mtunguja, nyanya, viazi, pilipili, na biringani.

Baadhi ya wagonjwa wanapendekezewa upasuaji unaohusisha kuingiza chombo fulani ndani ya kiungo chenyewe, na kuondoa utando unaotokeza vimeng’enya vinavyoharibu gegedu. Hata hivyo, mara nyingi uvimbe hurudi baada ya upasuaji huo.
 
Upasuaji wenye matokeo ya mara moja unahusisha kuondoa kiungo kizima (mara nyingi nyonga au goti) na kuweka kiungo kingine cha bandia. Mara nyingi maumivu huisha kabisa baada ya upasuaji huo, na viungo vya bandia hudumu kwa miaka 10 hadi 15.

Hivi majuzi madaktari wamejaribu matibabu ya kuingiza asidi fulani ndani ya kiungo. Magoti hasa hutibiwa kwa njia hiyo. Kulingana na uchunguzi mbalimbali huko Ulaya, matibabu ya kuingiza umajimaji mbalimbali unaotibu gegedu yamekuwa na manufaa kwa kadiri fulani pia.
 
Ijapokuwa ugonjwa wa yabisi-kavu hauna dawa, kuna dawa nyingi za kutuliza maumivu na uvimbe, na yaelekea baadhi ya hizo zinaweza kuzuia kwa kadiri fulani ugonjwa usizidi. Dawa zifuatazo ni dawa ambazo hutumiwa kutuliza dalili za yabisi-kavu: Dawa za kutuliza maumivu, dawa mbalimbali za cortisone, dawa zisizo na steroidi za kutibu uvimbe (NSAID), dawa za kupunguza dalili za ugonjwa zisizo za kutuliza maumivu (DMARD), dawa zinazozuia utendaji wa mfumo wa kinga za aina mbalimbali, na dawa nyinginezo. Hata hivyo, dawa hizo zote zinaweza kuwa na athari mbaya sana. Si jambo rahisi kwa daktari na mgonjwa kuchagua dawa inayofaa.
 
Back
Top Bottom