Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baridi-Yabisi

Mtu anaposhikwa na ugonjwa wa baridi-yabisi, mfumo wa kinga wa mwili huanza kushambulia viungo vyake kwelikweli. Kwa sababu isiyojulikana, chembe nyingi za damu—kutia ndani chembe za T, ambazo ni chembe muhimu katika mfumo wa kinga wa mwili—huingia ghafula katika vitundu vya kiungo. Jambo hilo husababisha utendaji mwingi wa kemikali ambao hufanya kiungo kifure.
 
Huenda chembe zinazotokeza umajimaji zianze kuongezeka kwa wingi sana, na kusababisha uvimbe unaoitwa pannus. Kisha uvimbe huo hutokeza vimeng’enya vinavyoharibu gegedu. Sasa kwa sababu mifupa inaweza kugusana, inakuwa vigumu kusogeza kiungo na hiyo husababisha maumivu makali sana. Misuli na kano pia hupoteza nguvu. Hiyo inafanya kiungo kianze kulegea na kuteguka kwa kadiri fulani, na mara nyingi kuharibika umbo.
 
Kwa kawaida ugonjwa wa baridi-yabisi huathiri viwiko, magoti, na miguu kwa wakati mmoja. Asilimia 50 hivi ya wagonjwa wanaougua baridi-yabisi hupata pia uvimbe au vinundu chini ya ngozi. Wengine wana upungufu wa damu, na wanaumwa na koo na macho makavu. Uchovu na dalili za mafua, kama vile homa na maumivu ya misuli, ni dalili nyingine za baridi-yabisi.
 
Si wagonjwa wote wanaougua baridi-yabisi walio na dalili zilezile, na hata muda ambao wagonjwa huugua hutofautiana vilevile. Huenda mtu mmoja akaanza kuumwa na kukakamaa polepole kwa muda wa majuma kadhaa au hata miaka. Lakini mtu mwingine anaweza kuwa mgonjwa ghafula. Baadhi ya watu huugua baridi-yabisi kwa muda wa miezi michache tu kisha wanapona kabisa. Wengine wanaweza kujisikia vibaya sana wakati fulani na kujisikia nafuu wakati mwingine. Na wengine wanaugua kwa miaka mingi, wakiendelea kulemazwa.
 
Ni nani hasa wanaoweza kupata ugonjwa wa baridi-yabisi? Dakt. Michael Schiff anasema kwamba “hasa wanawake wa makamo wanapata ugonjwa huo.” Hata hivyo, Schiff anasema pia kuwa “mtu yeyote wa umri wowote ule, watoto, na vilevile wanaume, wanaweza kupata ugonjwa huo.” Wale walio na watu wa ukoo wenye baridi-yabisi, wanakabili hatari ya kuupata kuliko watu wengine. Uchunguzi mbalimbali unaonyesha kwamba kuvuta sigara, kunenepa kupita kiasi, na kutiwa damu mishipani huzidisha hatari ya kushikwa na ugonjwa huo.
 
Yabisi-Kavu Aina ya Osteoarthritis

Jarida la Western Journal of Medicine lasema kwamba “ugonjwa wa osteoarthritis hufanana na hali ya hewa kwa njia nyingi—upo kila mahali, mara nyingi hautiliwi maanani, na nyakati nyingine una athari mbaya sana.” Ugonjwa wa osteoarthritis (OA) hutofautiana na baridi-yabisi kwa kuwa hauenei hadi sehemu nyingine za mwili bali huathiri kiungo kimoja tu au viungo vichache. Gegedu inapoharibika hatua kwa hatua, mifupa huanza kusuguana.
 
Back
Top Bottom