Chakula kilichotayarishwa katika viwanda na chakula chenye mafuta yenye asidi nyingi kiepukwe. Vyakula hivyo maalumu vinasaidia vipi? Inasemekana kwamba vyakula hivyo huzuia uvimbe. Wengine wanasema kwamba wamesaidiwa kwa kutokula nyama, vyakula vinavyotengenezwa kwa maziwa, ngano, na jamii ya mboga za mtunguja, nyanya, viazi, pilipili, na biringani.
Baadhi ya wagonjwa wanapendekezewa upasuaji unaohusisha kuingiza chombo fulani ndani ya kiungo chenyewe, na kuondoa utando unaotokeza vimeng’enya vinavyoharibu gegedu. Hata hivyo, mara nyingi uvimbe hurudi baada ya upasuaji huo.