Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

16. KABEJI

Imethibitika pasipo na shaka kuwa kabeji ni chakula bora kabisa ambacho kinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya aina mbalimbali za kansa, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, maambukizi mbalimbali, na mhimu kuliko yote ni kuwa kabeji inao uwezo pia wa kuzuia usipatwe na hamaki na mfadhaiko wa akili.
 
Kabeji lina vitamini B6, vitamini K na vitamini C. Ukiacha hayo kabeji pia ni chanzo kizuri cha folate, vitamini B1, potasiamu, copper, nyuzinyuzi (fiber) na manganizi. Viinilishe hivi ni mhimu sana katika kuichangamsha afya ya akili na mwili kwa ujumla.

Unaweza kutengeneza supu ya kabeji, juisi ya kabeji, kachumbali yenye kabeji ndani yake au ule tu mboga ya kabeji kila mara ili kupunguza stress yako bila gharama wala kutumia dawa yoyote yenye kemikali.
 
17. MAZOEZI YA VIUNGO

Mazoezi ya viungo ni dawa nyingine inayoweza kukuondoela msongo wa mawazo kirahisi zaidi bila gharama yoyote wala madhara yoyote katika afya yako.

Kuna watu mi nawaita kina chauvivu, kina chauvivu utawasikia ‘nakosa muda wa mazoezi’. Unakosa muda wa mazoezi mbona muda wa kulala hukosi? Huo ni uvivu tu ndiyo unakusumbuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…