Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
mwenyewe na kucheka zaidi. Mkasa niliokuwa nimeuona hata wewe ungekuweko ungecheka wiki nzima. Nilikuwa nimekatisha kwenye uchochoro mmoja ili niwahi kufika nyumbani, si unajua sie Wabongo kwa vichochoro ndio wenyewe, mambo ya kufuata barabara kama magari sie hatuwezi kabisa. Basi nikakatisha kichochoro kimoja, huko nikakuta kuna kelele ugomvi mkubwa unaendelea, watu walishaanza kukusanyika, kama kawaida ya Mbongo yoyote, lazima kujionea mweyewe kila tukio mubashara, nikajipenyeza kuona kulikoni.