Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ilivyo ndivyo ilivyo !!!
66c59d5209bdc191da87c9a47e9260c3.jpg
 
15. Kutafuna popoo, tambuu na mirungi.

Hii hupelekea meno kuwa na rangi isiyopendeza, meno hupoteza uimara wake na kutengeneza nyufa, mdomo kutoa harufu mbaya, huongeza uwezekanao wa kupata ugonjwa wa fizi, na ina kilevi kinachosababisha uteja (addiction). Matumizi ya vitu hivi hujenga tabia ya mazoea (addiction) ambayo inahitaji ushauri nasaha na matibabu kutoka kwa madaktari wa saikolojia
 
ENZI ZETU KABLA HAMJAZALIWA HATUKUWA WATU WA MCHEZO MCHEZO


Nakwambia siku hizi hakuna kitu, stori tu nyiingiii lakini vitendo hafifu. Madoido ndio mengii. Unajua zamani kabla wengi wenu hamjazaliwa watu tulikuwa sio wa mchezo mchezo. Mdogo akimkuta mkubwa anamwamkia Shikamoo, sio huu mchezo wenu eti mtoto mdogo anamwambia mkubwa
 
Heshima yako’, salamu gani hiyo? Yaani hivi mnaona aibu kuamkia ‘Shikamoo’? Enzi zile kabla hamjazaliwa mtoto alikuwa anamheshimu mkubwa yoyote yule, kma unamjua au humjui ukikosa adabu utakula mikwaju barabarani toka kwa mtu hata humjui wala yeye hakujui, na ukirudi kwenu husemi maana unaweza kuongezwa mikwaju. Watoto walikuwa wanaheshimu wakubwa, hakuna maswali wala demokrasia kuhusu hilo. Enzi hizo kabla wengi wenu hamjazaliwa kulikuwa hakuna
 
mchezo mchezo wa kusema eti msichana fulani gelfrendi wako, au mvulana boifrend wako, gelfrend au boifrend ndio nini? Hakuna hata neno la Kiswahili mnaishia kulisema Kiingereza, enzi zile kabla hamjazaliwa mtu ulikuwa na mchumba kwisha, yaani mpango wenu ni kuoana sio kuishia gesti. Hatukuwa watu wa mchezomchezo. Enzi hizo kabla hamjazaliwa mtu akikuudhi unamtafuta mnakutana
 
mbashara na anapewa kipigo chake au mipasho yake uso kwa uso, sio siku hizi anakuudhi mtu eti unaenda instagram kumpa vidonge vyake, kama sio dalili ya woga ni nini hicho? Enzi zetu kabla hamjazaliwa ukiona nimekutumia kitu kwa mtandao ujue hilo janga kubwa, watu ukiwaletea ujingaujinga walikuwa wanakutumia radi kwa mtandao wa kiasili, hapo ndio utajua wengine hawachezewi, na kama unajifanya unaringia pesa wanakutumia kitu kinanyonya pesa yako yote jeuri yako yote inaisha , hatukuwa
 
tunapenda mchezomchezo. Nakwambia enzi hizo kabla hamjazaliwa ilikuwa haitokei eti mtu kaiba mume au mke wa mtu, hakukuwa na facebook au sijui whatsapp ya kukutumia mipasho, mtu unaenda shtaki kwa babu yako halafu unangoja matokeo baada ya siku mbili, ndugu wa mgoni wako wanakugongea mlango kukuomba msamaha maana hapo ndugu yao kashushwa mshipa au kishakuwa chizi anaongea na mbuzi
 
mambo ya biashara. Hatukuwa wa mchezo mchezo. Enzi hizo kabla hamjazaliwa kulikuwa hakuna vibaka, mtu akikuibia unaloga ukoo mzima. Nimesema hatukuwa watu wa mchezo mchezo. Hatukuwa na gari wala baiskeli lakini tulikuwa tunatwanga kwa mguu Dar mpaka Moro kwenda kuhudhuria harusi tu. Hatukua watu wa mchezomchezo bwana
 
BINGWA WA NDOTO MUBASHARA

KILA binadamu ana mambo yake mengine ya ajabu sana ukihadithiwa huwezi kuamini. Kuna mshikaji wangu mmoja wanamuziki maarufu sana, ila ana ishu yake moja watu wangejua stori yake ndio ingekuwa kichwa cha habari cha kila gazeti. Mshikaji wangu huyu mtu mmoja smati sana kabla hajatoka nje ya nyumba yake lazima ajicheki kama yuko vizuri ndio anatoka nje.
 
Back
Top Bottom