Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

7. Kutafuna penseli au kalamu:



Tabia ya kutafuna penseli au kalamu inafanywa sana na watu wengi hasa wanapokuwa kwenye masomo, au kazi zinazohusisha kuandika, na wakati mwingine msongo wa kazi nyingi. Tabia hii huweza kupelekea meno kusagika kama itafanyika kwa muda mrefu. Kama unatabia hii ni vizuri ukatumia bazoka isiyo na sukari (sugarless gum), kila unapohitaji kutafuna kitu. Matumizi ya bazoka husaidia kuongeza na kusisimua mate kutoka mdomoni hivyo kuimarisha meno na hata kuzuia mashambulizi ya asidi.
 
8. Kuvuta sigara:

Matumizi ya sigara, na tumbaku za aina yeyote huweza kusababisha meno kubadilika rangi, na kuongeza uwezekanao wa kupata ugonjwa wa fizi. Pia matumizi ya tumbaku yanaweza kukusababishia kansa kwenye ulimi na mdomo. Tumia mbinu mbalimbali kukwepa na kuacha kabisa kuvuta sigara. Pamoja na madhara chungu nzima ya kiafya yanayoweza kusababishwa na uvutaji wa sigara, sigara haina faida yeyote katika mwili na maisha ya binadamu kwa ujumla.
 
3da4174f54a6a31192578e305bdd7437.jpg
 
9. Kutafuna barafu:

Kutokana na kuongezeka matumizi ya barafu na vinywaji baridi na vikali, baadhi ya watu hupendelea kutafuna barafu wakati wa kunywa vinywaji vyao. Kutafuna barafu kunaweza kusababisha meno kuvunjika, au kuweka nyufa zisizoonekana. Hii huweza kupelekea kupata maumivu au hali ya kufa ganzi wakati wa matumizi ya vitu vya baridi au vya moto. Pia barafu iliyovunjika inaweza kuwa imechongoka na kuweza kusababisha kidona kwenye fizi na ulimi. Inashauriwa badala ya kutafuna barafu, iache iyeyuke mdomoni, kama wewe unapendelea raha ya ubaridi wa barafu mdomoni kwako.
 
10. Kusaga na kutafuna meno (Bruxism)

Kusaga na kutafuna menoKusaga na kutafuna meno ni tabia inayohusisha msuguano wa meno unaotokea wakati wa usiku au hata mchana, na hupelekea meno kusagika, kulika na kuweka nyufa ndogo ndogo kwenye sehemu ngumu ya jino, na kuumwa kwa misuli ya uso na viungo vya taya. Pia meno huweza kupata ganzi mara kwa mara na kupata shida ya kutafuna. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kutumia kizuizi kinachoitwa “night guard” wakati wa usiku na ushauri nasaha kutoka kwa daktari wa afya ya kinywa. Ganzi kwenye meno inaweza kutibiwa kwa kupaka dawa maalumu inayozuia ganzi pamoja na kutumia dawa ya meno inayopunguza ganzi (toothpaste special for sensitive teeth)
 
11. Matumizi ya chupa za lishe kumlazia mtoto:

Hii itamfanya mtoto awe anategemea kulala akiwa na chupa mdomoni–ya juisi, maziwa au lishe yoyote. Matumizi ya chupa hizi bila mpangilio yanaongeza uwezekano wa kuoza meno kwa kasi (rampart caries). Inashauriwa chupa hizi zitumike kwa matumizi ya lishe tu, na sio kitu cha kumbembelezea mtoto alale usingizi.
 
12. Kutoga ulimi, mdomo, mashavu:

Kutoga ulimi kunaweza kusababisha kuvuja kwa damu nyingi pale mshipa mkubwa wa damu utakapotobolewa. Pia kidonda kisipotunzwa vizuri huweza kupata maambukizi na kushindwa kupona kwa wakati. Kipini cha urembo kinachowekwa kwenye ulimi, mdomo au mashavu kinaweza kupelekea jino kuvunjika pale kiking’atwa kwa bahati mbaya– au kutengeneza nyufa ambazo zitakuwa zinauma na hata kusababisha ganzi kila unapokula kitu cha baridi, cha moto, au hata hewa ya baridi ikiingia mdomoni.
 
13. Matumizi ya tembe za kulainisha koo (throat lozenges):

Tembe hizi mara nyingi huwekwa kiwango kikubwa cha sukari hivyo kukuongezea hatari ya kuoza kwa meno. Tabia ya matumizi ya chembe kama kiburudisho ni hatarishi kwa afya ya meno. Matumizi yasioyo sahihi, ni matumizi ya mara kwa mara yasiyohitajika. Tembe hizi zikitumika kwa muda mfupi hazina madhara yoyote kwenye meno.
 
13. Matumizi ya tembe za kulainisha koo (throat lozenges):

Tembe hizi mara nyingi huwekwa kiwango kikubwa cha sukari hivyo kukuongezea hatari ya kuoza kwa meno. Tabia ya matumizi ya chembe kama kiburudisho ni hatarishi kwa afya ya meno. Matumizi yasioyo sahihi, ni matumizi ya mara kwa mara yasiyohitajika. Tembe hizi zikitumika kwa muda mfupi hazina madhara yoyote kwenye meno.
 
14. Matumizi mabaya ya mvinyo:

Mvinyo una kiwango kikubwa cha asidi ambayo huaribu sehemu ngumu ya nje ya jino inayoitwa enameli na kuacha matundu madogo kwenye meno yanayosababisha kuhifadhi vitu vinavyoweka rangi kwenye meno. Mfano, mvinyo mwekundu una chembechembe zinaitwa “chromogens” pamoja na “tannins” ambavyo huweka rangi kwenye meno. Wanywaji wengi wa mvinyo hunywa taratibu kwa muda mrefu, hivyo kufanya asidi ya kwenye mvinyo hivyo kufanya tindikali (acid) iliyomo kwenye mvinyo iharibu meno. Pia tindikali hiyo husababisha kumomonyoka kwa enameli (dental erosion), na kuifanya kuwa dhaifu. Kama meno yako yameathirika kwa kuwa na rangi isiyokuridhisha na wakati mwingine kufa ganzi kutokana na kumomonyoka kwa enameli na unafikiri imetokana na matumizi ya mvinyo kama maelezo hapo juu, basi punguza matumizi haya na pata ushauri wa daktari wa kinywa na meno kutibu tatizo la ganzi
 
15. Kutafuna popoo, tambuu na mirungi.

Hii hupelekea meno kuwa na rangi isiyopendeza, meno hupoteza uimara wake na kutengeneza nyufa, mdomo kutoa harufu mbaya, huongeza uwezekanao wa kupata ugonjwa wa fizi, na ina kilevi kinachosababisha uteja (addiction). Matumizi ya vitu hivi hujenga tabia ya mazoea (addiction) ambayo inahitaji ushauri nasaha na matibabu kutoka kwa madaktari wa saikolojia
 
Back
Top Bottom