Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inakadiliwa kuwa mwanamke anayejifungua inamchukua miaka miwili kurejesha gram moja ya madini chuma yaliyopotea toka mwilini wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo.
 
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kukabiliana na tatizo hilo:

• Kula vyakula vyenye madini chuma na zinc kwa wingi kama vile maharage, korosho, mboga za majani hasa spinach, mayai, nyama, samaki, mbegu za maboga na matunda.
 
Usinywe vinywaji vyenye caffeine wakati wa kula chakula.
• Meza dawa zinazoongeza madini chuma mwilini kama vile ferrous sulfate nk.
• Safisha misumali kwa maji moto, iloweke kwenye maji ya limao kisha tengeneza juice kwa maji haya na unywe mara kwa mara au pika chakula kwa kutumia sufuria ya chuma.
 
1. Kutafuna kucha

Tabia hii inaweza kusababisha sehemu ya jino kusagika, kuwa dhaifu na hata kuvunjika. Pia na matatizo katika viungo vya taya na hivyo kuleta maumivu karibu na eneo la masikio (Temporomandibular joint dysfunction). Chanzo cha tabia hii chaweza kuwa ni mazoea tu, au msongo wa mawazo, kazi, n.k. Ili kuacha tabia hii kata kucha kwa kutumia kifaa maalumu kwa wakati, epuka msongo wa mawazo, kuwa na mpangilio mzuri wa kazi zako.
 
2. Kupiga mswaki kwa kutumia nguvu

Usitumie nguvu sana kupiga mswaki, kwani unaweza kusababisha kuharibika kwa fizi zako na sehemu ya jino inayopakana na ufizi. Tumia mswaki wenye brashi laini, na muda wa wastani wa dakika mbili, mara mbili kwa siku.
 
3. Kutumia meno yako kama kifaa



Tabia kama kufungua kizibo cha chupa, kufungua pakiti ngumu kama za maziwa kwa meno, kushika vitu kama sindano, kushikilia au kumenyea nyaya (kwa mafundi wa umeme, betri), kushikilia misumari (mafundi ujenzi),n.k. Kazi ya meno ni kutafuna chakula sio kutumika kama kifaa mbadala. Tabia hizi huweza kupelekea kuvunjika meno, au kujiumiza mdomoni, au hata kumeza vitu hivyo kwa bahati mbaya.
 
4. Tabia ya kutafuna vitu vigumu kama mchele,

Hii husababisha meno kusagika au kuweka nyufa na maumivu au ganzi kwa baadhi ya meno na hata kuvunjika kwa kipande cha jino. Tabia hii huanza taratibu kwa kuiga na baadae kuwa mazoea. Kuwa mbali na vitu hivyo vinavyotamanisha kutafuna kunaweza kusaidia kuacha tabia hii.
 
5. Kula vitu vyenye sukari mara kwa mara:

Kula kashata, ufuta, ubuyu, visheti, biskuti, pipi, keki, bazoka (Big G, orbit, n.k.) mara kwa mara, hasa vile vyenye sukari huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kuoza kwa meno. Mabaki ya vyakula hivi hutumiwa na bakteria (wanaoozesha meno) kutengeneza asidi inayoharibu sehemu ngumu ya nje ya jino na kuacha matundu. Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari, njia mojawapo ikiwa ni kuvitumia vyakula hivyo wakati wa unapokula milo mikuu mitatu
 
0d31bf87c8e75247b7df7afa96694ec0.jpg
 
6. Matumizi ya kahawa:

Rangi ya kawaha huweka rangi kwenye enameli (sehemu ngumu ya nje ya jino) na asidi iliyopo ndani yake huweza kusababisha enameli kulika, hivyo rangi ya asili ya meno kupungua na kuanza kuwa na rangi ya njano kadiri muda unavyopita.
 
Back
Top Bottom