Miwani ilikuwa inauzwa 99 cents - $15 kutegemea na design. Tena kwenye gas stations tu. Amazon huko pia ilikuwepo ya kutupwa. Problem watengenezaji hawakutengeneza mingi. Hapa katikati media wakaanza kupiga debe kuwa total eclipse hii ni ya mwisho kwa kila aliyeko hai kwa sababu nyingine ingetokea baada ya miaka 99. Basi ikawa ni event kubwa ambayo ilikuwa lazima kila mtu aone. Glasses za 99 cents zikaanza kuuzwa 10 bucks na kuendelea. Hoarders na price gaugers wamepiga hela nzuri. Wengine walipoona upungufu wakaanza kutengeneza za kwao feki na kuziuza haraka haraka mtandaoni. Dogo mmoja kapiga $30,000 kwa kuuza basically plastic nyeusi tu akidai ni NASA certified glasses. Waliozinunua na kuzitumia tayari macho yanawauma na moto umeanza kumwakia sijui itakuwaje.
Hizi ni opportunity zinazokuja bila kutegemewa na wenye jicho la ndani ndo wanaweza kuziona.
Pamoja na demands yote hii public library nyingi zilikuwa na stock ya miwani 500 kila moja na anayewahi kabla hazijaisha anapatiwa bure. Mwenyewe nilikwenda kwenye library nikapiga mstari nikapata tena pea mbili. Hakuna kusukumana wala nini.