Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kawaida kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali vyenye kuleta athari kwa afya kama vile vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na virusi, lakini wakati mwingine pia na vitu ambavyo havina madhara yoyote kwa mwili, ambavyo huitwa allergens (mzio).
Mtaalamu wa dawa na tiba kutoka hospitali ya Sanitas, Dk Sajjad Fazel anasema aleji au mzio (allergy) ni matokeo ya kinga ya mwili inapofanya kaz
 
ya ziada ya kupambana na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili pale inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.
“Kinga ya mwili inapoamua kufanya kazi ya ziada husababisha mtu kuwa na dalili za aleji au mzio katika mwili wake kwa kuona dalili mbalimbali”, alisema Dk Fazel.
Vitu vinavyosababisha mzio
Dk Fazel anasema baadhi ya vitu vinavyosababisha mzio ni pamoja na vumbi, baadhi ya
 
dawa zenye madini ya sulfer, vyakula, kung’atwa na wadudu kama vile nyuki na baadhi ya uyoga.
Anasema wapo pia watu ambao wanapatwa na mafua karibu kila siku na wengine kushindwa kuvaa aina fulani ya nguo na vitu kama saa,hereni na cheni, kwani mara nyingi husababisha kuwashwa na kuvimba mara wavivaapo.
Anasema watu wenye mzio huwa na hisia zisizo za kawaida za mwili dhidi ya vitu vinavyowaathiri na pindi mwili
 
unapokumbana na vitu vinavyosababisha mzio, mfumo wa kinga wa mwili huzalisha kemikali mbalimbali, mfano histamine ambazo hupambana na mzio.
Mara nyingine watu hupata ugonjwa wa mzio pindi wanapokutana na aina fulani ya mazingira kama yenye vumbi, baridi ya wengine hupatwa na mzio wanapopigwa na jua kali au msuguano wa ngozi unaweza kuwasababishia dalili fulani za mzio.
 
Dalili zake
Dk Fazel anasema mara nyingi dalili hutegemeana na mgonjwa ana aina gani ya mzio.
Kama mtu atakuwa na mzio katika mfumo wa hewa, huweza kupata matatizo ya kupumua anapokutana na mazingira yenye vumbi, hali inayomsababishia kupiga chafya mara kadhaa, kutokwa na makamasi, kuziba pua, muwasho kwenye pua na koo au kupumua kwa kutoa sauti kama filimbi, kuumwa na kichwa mara kwa mara, kizunguzungu, pumu, kuhisi joto katika mwili na mfadhaiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…