Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

dunia (Stephen Hawking), sisi ni viumbe tulioumbwa kwa mfano wa Mungu na inatupasa kuakisi tabia yake na kuonesha wema na uwezo wake wakati sisi wenyewe tukistaajabu katika uwezo na wema na kukua na kukomaa humo. Tukitambua kuwa tumeumbwa kwa sababu maalum, tunaona umuhimu na makusudi, ikiwa ni pamoja na afya na uzima, kwa kuyatafuta na kuyafuata makusudi na matakwa ya Mungu kwa ajili yetu.
 
Uzima mchanganyiko
Pamoja na kufundisha kuwa tulikusudiwa kuwa tulivyo, Kitabu cha Mwanzo pia kinaonesha tulivyo. Kinyume na mtazamo wa kale wa kipagani unaotenganisha mwili na roho katika maeneo tofauti (mwili ukiwa mwovu na roho njema), Maandiko yanafundisha kile ambacho wengine wanakiita “uzima mchanganyiko”, dhana ya kwamba vipengele vyote vya mwanadamu – kimwili, kiakili
 
na kiroho – vinaunda kitu kimoja, na hakuna kipengele kinachoweza kuwepo bila kingine. Mungu alipompulizia Adamu pumzi ya uhai, Biblia haiseami kwamba Adamu alipokea nafsi, kana kwamba roho ilikuwa kitu tofauti na yeye, bali alikuwa “nafsi hai” (nephesh hayah). Alikuwa nafsi hai, hakuwa nafsi hai. Ajabu ni kwamba, Biblia inatumia kirai hicho hicho kwa wanyama pia: “Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai (nephesh hayah)
 
kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao” (Mwanzo 1:21 soma pia aya ya 24). Ingawa bila shaka Adamu alikuwa tofauti na nyangumi na kobe kwa namna nyingi, lakini alikuwa nafsi hai kama wao, nephesh hayah.
Kuelewa hivyo kunaweza kutulinda dhidi ya aina mbili za kuvuka mpaka. Ya kwanza, inaitwa duaslism inasisitiza zaidiupande wa kiroho na hata kutweza vitu vinavyoonekana kuwa ni viovu. Hata hivyo kuanzia Mwanzo na kuendele
 
ambapo Mungu aliona kuwa dunia iliyokuwa imekamilika ilikuwa njema sana (Mwa 1:13), Maandiko yanachukulia kuwa vitu vilivyomo ulimwenguni ni matokeo ya uwezo wake wa kuumba. Hata miili yetu, ingawa imeanguka, bado ni viumbe vya Mungu nab ado inahitaji kuheshimiwa hivyo: “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe?” 1 kor. 6:19).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…