Faida ya mazoezi haya ni pamoja na kuchoma mafuta yaliyorundikana, kuimarisha afya ya moyo na mapafu hivyo kukufanya kuwa na upumuaji mzuri na mzunguko imara wa damu.
Pale unapofanya mazoezi kila mara na kwa muda mrefu ndivyo pia mwili unatumia zaidi mafuta yaliyorundikana hivyo kuwezesha kudhibiti unene/uzito mkubwa.
Hivyo kuanzishwa kwa utaratibu wa kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya mwezi na Serikali ichukuliwe kuwa ni kichochezi cha kutufanya kupenda kufanya mazoezi mepesi.
Isije ikatokea kuwa unafanya tu mazoezi hayo katika siku hiyo tu ilyoelekezwa, utakuwa unajidanganya kwani ili kuweza kupata afya njema inahitajika kujenga tabia ya kufanya mazoezi mepesi mara kwa mara kwa muda mrefu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.