Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Magonjwa huwakumba zaidi watu wenye kipato kizuri kutokana na tabia yao ya kutozingatia lishe bora. Wananchi wa mataifa yaliyoendelea wapo kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa haya. Licha ya ulaji holela, watu hawa hawafanyi mazoezi kama inavyoshauriwa. Wanakula zaidi vyakula vya wanga na mafuta, wanakunywa pombe na kuvuta sigara bila kujali athari zake.
 
Magonjwa huwakumba zaidi watu wenye kipato kizuri kutokana na tabia yao ya kutozingatia lishe bora. Wananchi wa mataifa yaliyoendelea wapo kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa haya. Licha ya ulaji holela, watu hawa hawafanyi mazoezi kama inavyoshauriwa. Wanakula zaidi vyakula vya wanga na mafuta, wanakunywa pombe na kuvuta sigara bila kujali athari zake.
 
Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea baada ya sehemu ya nyama ya moyo kuharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha. Yote yanaweza kusababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye moyo kutokana na mafuta mwilini.
 
Wengine ni wagonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, wenye unene wa kupitiliza au kitambi na wenye matatizo ya figo. Wanywaji wa pombe kupindukia na wanaotumia dawa za kulevya pia hasa cocaine na methamphetamine. Wengine ni wenye msongo wa mawazo wa muda mrefu au upungufu wa vitamin B2,B6, B12 na folic acid.
 
Dalili

Maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto ni dalili za awali. Kupumua kwa shida na kutokwa jasho kwa wingi au kuhisi mapigo ya moyo kwenda haraka. Kichefuchefu, kutapika na kuchoka haraka pamoja na kupoteza fahamu. Vichomi hasa vinavyosababishwa na vimelea vya chlamydophila pneumonia. Tafiti mbalimbali zinalihusisha shambulizi la moyo na msongo wa mawazo.
 
Matibabu

Shambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharura. Lisipotibiwa kwa haraka huweza kusababisha kifo ndani ya muda mfupi tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha kumuongezea mgonjwa oksijeni na kupewa vidonge vya Aspirini ndogo vinavyozuia damu kuganda pamoja na kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyoziba.
 
Kujikinga

Zipo njia kadhaa za kujikinga na shambulio la moyo ambazo zinajumuisha kutovuta sigara, kufanya mazoezi ya mara kwa mara na kupunguza unywaji pombe. Kubadilisha aina ya mlo kwa kupunguza mafuta na chumvi, kutumia mafuta ya samaki zaidi na baadhi ya tafiti zinasema uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.
 
Madhara

Kifo kinaweza kutokea endapo moyo utashindwa kufanya kazi. Upo uwezekano wa shambulio la moyo kurudia mara ya pili.

Ili kutambua tatizo hili, mwaka 1979, Shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vinavyojumuisha maumivu ya kifua kwa Zaidi ya dakika 20.
 
Nikiwa mmoja wa waunga mkono katika juhudi za kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza yaani non-communicable disease leo nitawapa dondoo zinazohusu mazoezi mepesi.

Kama ilivyoendelea kuelezwa na serikali kuwa kutakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya mwisho
 
Mazoezi mepesi ni pamoja na kukimbia mbio za taratibu, kutembea, kuogelea, kuruka Kamba, kufanya kazi ndogo ndogo, kuendesha baiskeli na kucheza mziki.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zimebaini kuwa mazoezi mepesi ndiyo yanayochangia watu kuishi maisha marefu zaidi. Hii ni hutokana na mazoezi haya kumuepusha mtu na magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu na unene uliopitiliza.
 
Faida ya mazoezi haya ni pamoja na kuchoma mafuta yaliyorundikana, kuimarisha afya ya moyo na mapafu hivyo kukufanya kuwa na upumuaji mzuri na mzunguko imara wa damu.
Vilevile hukusaidia kukupa mwili makakamavu na utulivu wa kiakili na kimwili.

Mazoezi haya yanakufanya kuepukana na msongo wa mawazo ambalo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…