Katika utafiti uliofanywa na Star Tv jijini Mwanza kwenye makundi mawili ya watu kumi, kati ya watu wanne kwa kila kundi wanatumia simu za stmartphone kwa kutafuta habari na biashara, hii inamaanisha katika makadirio ya utafiti huu kwa kila watanzania kumi, wanne hutumia smartphone kwa matumizi sahihi na sita kati yao hutumia simu kwa kucheza kamali, kutafuta nyimbo, wachumba, kupashana michapo maarufu kama umbea na kutazama picha na kusikiliza sauti zinazochochea ngono.