Hana moral authority yoyote lakini alichokisema kina ukweli mkubwa sana na muhimu sana kwa Taifa letu kwa sasa na siku za usoni. Hata kichaa akikwambia nilimuona mtu anataka kuchoma nyumba yako unaweza kumpuuzia kwamba yule kichaa tu ni hawezi kusema chochote chenye maana lakini kumbe anasema ukweli mtupu. Mkuu tusiyadharau maneno ya Kikwete kwa sababu hana moral authority njia yetu iko njia panda sasa hivi ni matumaini yangu wastaafu wengi, viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla wenye mapenzi ya kweli kuhusu nchi yetu wasimame kidete ili kukataa hizi chuki, visasi vya kutisha vinavyoshamiri nchini mwetu before it is too late. Kwa faida yetu na vizazi vijavyo.
Kumbuka Kikwete si wa kwanza kuikemea hii Serikali/huyo aliye Ikulu, Mwinyi, Warioba, Kinana, Butiku nao wamewahi kufanya hivyo kwa nyakati tofauti. Mdharau mwiba.....