Sasa kusema ukweli tangu lini ikawa chuki? Ingekuwa namsingizia mambo hapo ungesema ukweli. Hata CAG kaandika kuhusu ufisadi wa huyu katika ripoti tatu tofauti. CAG naye kwa kuandika ukweli kuhusu huyu ana chuki dhidi ya dikteta uchwara? Kikwete naye ana chuki dhidi ya dikteta uchwara? Hebu acha hizo Mkuu. Matendo yake na kauli zake mwenyewe huyu ndiyo chanzo cha utawala wake kuingia dosari kubwa sana na si chuki za yoyote yule.
Ukweli kuhusu huyu dikteta uchwara na nduli ni lazima usemwe bila kupindisha hata chembe kwa faida ya Tanzania ya sasa na vizazi vyetu vijavyo.
Ben Saanane kishapotea kwa kosa lipi? la kusema huyu dikteta uchwara Phd yake ni Phd uchwara? Watanzania wangapi wapotee nchini ndiyo tuanze kumshinikiza huyu na chuki zake za kutisha na visasi?