Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Epuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi. Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi huongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu na baadhi ya aina ya saratani. Matumizi ya chumvi nyingi huweza kupunguzwa kwa kutumia kidogo wakati wa kupika, kuepuka vyakula vyenye chumvi nyingi au vilivyosindikwa kwa chumvi. Pia, jenga tabia ya kutoongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula.