Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Epuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi. Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi huongeza uwezekano wa kupata shinikizo kubwa la damu na baadhi ya aina ya saratani. Matumizi ya chumvi nyingi huweza kupunguzwa kwa kutumia kidogo wakati wa kupika, kuepuka vyakula vyenye chumvi nyingi au vilivyosindikwa kwa chumvi. Pia, jenga tabia ya kutoongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula.
 
Kunywa majisafi, salama na ya kutosha. Kunywa maji angalau glasi nane (lita moja na nusu) kwa siku. Maji ni muhimu mwilini kwani hurekebisha joto la mwili, husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, husafirisha virutubisho kwenda kwenye seli na huondoa mabaki au uchafu mwilini kwa njia ya jasho na mkojo. Vilevile maji husaidia kulainisha maungio ya mwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…