Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jibu likamjia. Akakumbuka ni nini Hezron alimwambia. Kwamba mkewe yawezekana amekufa kwa shinikizo la damu kutokana ma stress. Kwa hali hiyo Daniel nimemuua mke wangu.

"Nimemuua mke wangu mwenyewe. Mungu nisamehe…" alijutia huku akiendesha gari kwa kasi.

Daniel akakumbuka jinsi mambo yalivyoenda vibaya katika ndoa yake. Jinsi gani upendo ulikimbia katika ndoa yao. Jinsi gani walivyoanza mabishano na ugomvi. Takribani mara nne ameshampiga mkewe vibao. Alikuwa mtu mbaya kwa mkewe na kwa watoto wake wadogo wawili.
 
Alifikiri aache kuhudumia familia, hitaji lake likaja kuwa kutomheshimu mkewe, kutomheshimu mkewe kukaleta dharau na maneno ya kejeli kwa mkewe, maneno ya kejeli yakasababisha vidonda vya tumbo kwa mke mwema Lisa kutokana na mawazo na kutokula.

Naam, Lisa aliugua vidonda vya tumbo kutokana na maumivu ya mawazo aliyosababishiwa na mumewe. Afya yake ilikongoroka, umbo lake zuri namba nane lilipotea, Lisa alionekana kama mzee, wakati ni mwanamke wa miaka 29 tu. Ila Daniel hakujali, alimzarau. Alijibadili kutoka mume aliyempenda mkewe kuwa mtu msaliti, anayemuumiza mkewe. Lisa amefariki!!?
 
Akiwa bado anaendesha akakumbuka jinsi alivyomfuata Lisa na kumuomba wafunge ndoa, Lisa alikuwa mzuri, akijitegemea na mwenye furaha na maisha. Yeye kumuoa tu ndio ikawa kumharibu, kumuumiza na mwishowe kumuua kwa stress!

Atakufaje? Hawezi kujua kwa sababu hajarudi nyumbani wiki moja sasa imepita, hajui watoto wanakula nini, wanavaa nini. Mke wake alikuwa akimtumia texts na kumpigia akimsisitizia arudi nyumbani, ila kilio cha mkewe kilitua katika masikio yake ambayo hayasikii. Mkewe alikuwa akilia, akipiga kelele mumewe arudi nyumbani, yote hayo ni kwa ajili ya kuokoa ndoa yake. Lakini mimi Daniel sikusikia. Sasa amefariki!
 
Mimi nitafanya nini na watoto wangu?" alifikiria nafsini kwake. Watoto wawili alionao ambao alikuwa hawajali kwa sababu ya kuwa busy na warembo wa jiji la Makonda. Akakubali kwamba kweli mke wake alikuwa na moyo wa ajabu, kuwatunza watoto wale wawili bila msaada wake.

"Nani atanisaidia kuwalea? " Wanawake ambao amekuwa akila nao bata hawawezi kumsaidia kulea watoto, sio wife material wale, wife material hawezi kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake. Alifikiria nafsini mwake.
 
Wazazi wa mkewe watafikiri nini?
Watu watafikiri nini? Mungu ananifikiriaje?
Hii ndio inaishaje ishaje? Ndoa yangu ndio imeishia hivi? Mke wangu kafariki?

Daniel akapaki gari, akatoka na kukimbia ndani ya nyumba.

Akafungua geti, akafungua mlango. Akamuona Hezron, rafiki yake akiwa amesimama katika korido ya nyumba yake.

"Kimetokea nini? Haiwezekani kuwa amekufa. Hawezi kufa. Mimi nitafanya nini Hezron?" Daniel aliongea akiwa amekata tamaa.
 
Hezron akamkumbatia Daniel.

"Uko sawa Daniel?" Hezron aliuliza.

"Nitakuaje sawa wakati mke wangu amekufa? Mama wa watoto wangu! Uko wapi mwili wake?" Daniel aliuliza.

"Upo sebuleni" Hezron alijibu.

Daniel akakimbia kuelekea sebuleni.

Mshangao!!

Akamwona mkewe akiwa hai. Amekaa katika sofa akiwa na mke wa Hezron ambae ni daktari wa saikolojia pembeni.
 
umechanganykiwa eeeh! sa skia
kwanz
mi nna boyfriend wang ananipenda
ana
magar na mifweza tele tna hawez
n2mia
buk 2 so ctak uxumbuf niachee!!!
JAMAA:{Huku akshusha pumz}
xamahan
xana ila nilkuwa nko show room
nakununulia [HASHTAG]#gar[/HASHTAG] sa nme2ma elf 2
m_pesa ili nipat jna lako kamik il
nkuxajilie gari lako,poa mxalimie
shemej!!!
DEMU:{Huku akjichekesha}baby,
honey,my darling jaman sweetie
hutaniw ????mi nakutania mwaya!!!!
JAMAA:{Kakata cm zaman…..!!}
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Haujafa?!" Daniel aliuliza akiwa na mshangao

"Ndio hajafariki. Ila kama ukiendelea na hii tabia atafariki siku moja. Mkeo hajawa sawa kabisa. Amekuwa akijaribu kukutafuta na kukurudisha nyumbani ila umempuuza. Taarifa za kifo chake zimekufanya ukimbie kama mwehu. Ulitakiwa ukimbie kwa ajili ya maisha yake na si kwa ajili ya kifo." Mke wa Hezron aliongea.

Daniel akakaa katika kochi mbele ya mkewe na akamshika uso wake. Mkewe akarudishwa kichwa nyuma.
 
Natumaini kwamba safari yako ya uchungu kuja hapa ukifikiri mkeo amekufa itakukumbusha ni nini cha muhimu kinachotakiwa kufanywa. Usisubiri mpaka uchelewe ndio ufanye jambo jema. Unayo nafasi ya pili." Aliongea mke wa Hezron

Daniel akanyanyua mkono wa mkewe machozi yakimtiririka, asiamini juu ya kile anachoshuhudia.

"Ndoa sio lelemama nyie wawili. Acheni kucheza michezo ya kipumbavu na maisha. Kesho sio garantii" aliongeza mke wa Hezron.
 
Nyie wawili mna matatizo. Mmeridhika na matatizo ya kuumizana hasa wewe shemeji yangu Daniel. Kesho haiwezi kuwa pale kwa ajili yako kwa ajili ya kuomba msamaha. Mkewe Hezron aliongea.

"Na siku ya kiama tutakapokutana na mwenyezi Mungu, Daniel kitu ambacho Mungu atauliza ulimtendaje mke wako ambae ni ubavu wako? Huyu ni binti wa Mungu. Unavomuumiza yeye na Mungu anaumia pia" Akaongezea Hezron.
 
5e65c925d5e152ff1be9b31c903d39be.jpg
 
Back
Top Bottom