Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Misingi mitano muhimu ya biashara.
Ili biashara yoyote iweze kudumu na kukua inahitaji kufuata misingi ifuatayo.

Kutengeneza thamani.
Ili biashara iweze kukua na kutengeneza faida ni lazima itengeneze bidhaa au huduma ambayo ni ya thamani kwa wateja. Ni lazima utoe bidhaa au huduma ambayo watu wanaihitaji sana ili kuboresha maisha yao. Kama hujaanza biashara fikiria ni kitu gani cha thamani ambacho watu wanakihitaji ila wanakikosa, kisha anza kuwapatia na utajenga biashara kubwa. Kama tayari unafanya biashara angalia ni kitu gani cha thamani unachotoa kwa watu na angalia jinsi unavyoweza kuboresha ili kupata wateja wengi zaidi.
 
Soko.
Kuwa na kitu chenye thamani pekee bado haikutoshi kutengeneza biashara kubwa, ni lazima kuwe na soko linalohitaji bidhaa au huduma hiyo. Hata kama soko lipo bado sio rahisi kwa kila mtu kujua kwamba unatoa huduma muhimu. Hivyo ni muhimu kutafuta soko la biashara yako kwa njia mbalimbali zikiwemo matangazo. Inakubidi uhakikishe watu wanajua uwepo wa biashara yako na utengeneze uteja ili watu waje kupata thamani unayotoa. Kukosa soko la uhakika ni chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.
 
Kuuza.
Ili biashara ikue ni lazima uweze kuuza thamani uliyotengeneza. Ni muhimu uweze kuwashawishi watu wanunue bidhaa au huduma unayotoa. Kuuza ndio moyo wa biashara ambapo kama usipokuwa makini ni rahisi kwa biashara kufa.
 
Kufikisha thamani.
Kama umewaahidi wateja wako kwamba bidhaa ama huduma unayotoa itaboresha maisha yao basi hakikisha hicho ndio kitu kitakachotokea kwa wateja. Ni lazima uweze kufikisha thamani uliyoahidi kwa wateja. Kwa kushindwa kufanya hivi wateja watakuona wewe ni tapeli na hawatanunua tena bidhaa yako. Kama biashara itashindwa kutengeneza wateja wanaojirudia ni lazima itakufa.
 
Fedha.
Usimamizi wa fedha ni muhimu sana kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.
 
Fedha.
Usimamizi wa fedha ni muhimu sana kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara nyingi.
 
Misingi hii mitano ni muhimu sana kwa biashara. Hakuna msingi ambao unaweza kusema ni muhimu zaidi ya mwingine, yote inategemeana. Ili biashara yoyote iweze kudumu ni muhimu kuzingatia misingi hiyo.
 
ili uweze kufanya kazi vizuri na wafanyakazi wako na biashara yako iweze kukua.

Tengeneza utamaduni wa kufanya kazi kama timu.
Kuna faida kubwa sana kwenye timu, kwa sababu watu wote hatulingani au kufanana, basi tunahitaji kusaidiana kwa hali ya juu. Kuna mtu ambaye ni mzuri kwenye jambo fulani na mbovu kwenye jambo jingine. Mtu huyu anapokutana na mwingine ambaye anafukia mapungufu yake, biashara yako inakwenda vizuri sana.
 
Hakikisha wafanyakazi wako wanafanya kazi kwa kushirikiana na wanajua wote lengo lao ni moja ambalo ni mafanikio ya biashara. Kwa kushirikiana huku pamoja na wewe mnaweza kuleta mabadiliko makubwa.
 
Tambua michango ya wafanyakazi kwenye ukuaji wa biashara yako.
Pamoja na kutoa kipato kizuri, binadamu hawavutiwi na kipato pekee, bali wanapenda kuona wakithaminiwa kwa kile wanachofanya. Tambua michango ya wafanyakazi wako kwenye ukuaji wa biashara yako, na wapongeze na kuwashukuru kwa juhudi zao. Unaweza kufanya hivi kwa kuweka nao malengo pamoja na yanapofikiwa wakapata zawadi fulani au hata kutambuliwa kwa kazi yao bora. Kwa vyovyote vile hakikisha wanajisikia ufahari kuweka juhudi zaidi.
 
Wasaidie wafanyakazi kujiongoza wenyewe.
Ni kawaida kwa mmiliki wa biashara kutaka kumsimamia mfanyakazi kwa karibu sana. Unaweza kufanya hivi ila hii itakuchukulia muda wako mwingi na hivyo utashindwa kukuza biashara yako. Pia wafanyakazi wako ni watu wazima, na hakuna mtu mzima anayependa kuona anafuatiliwa kwa kila kitu.
 
Wajengee wafanyakazi kujiamini na sio hofu.
Waajiri wengi wamekuwa wanajenga hofu kubwa kwa wafanyakazi wao. Watu wanahofia wakifanya jambo fulani au wakishindwa kufanya jambo fulani watafukuzwa kazi. Hii inawafanya watawaliwe na hofu na hivyo kushinda kufanya mambo makubwa na mazuri.
 
overloaded-truck7.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamwe usiwatishie wafanyakazi kwamba utawafukuza kama ndio njia ya kuwafanya watekeleze majukumu yao, hivyo unawajengea hofu. Kama kuna wafanyakazi ambao hawatimizi majukumu yao, kaa nao na ujue tatizo ni nini. Wakati mwingine hawana uelewa halisi wa kazi yao. Wajengee kujiamini na kuamini kwamba wanaweza na watakufanyia kazi nzuri sana.
 
Makosa ni sehemu ya kujifunza.
Jambo jingine muhimu sana unalotakiwa kufanya wewe kama mwajiri ni kuchukulia makosa wanayofanya wafanyakazi wako kama sehemu yao ya kujifunza. Usitoe adhabu kubwa kwa wafanyakazi wanaokosea, ila jua hilo ni darasa zuri kwao na wakati mwingine hawatarudia tena.
 
Back
Top Bottom