Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6850d744a1472bca344cfc7d8cfab957.jpg
 
miongoni mwa wanyama wenye sumu kali namba moja inachukuliwa na huyu ambaye anaitwa BOX JELLY FISH (kwa jina la kizungu).BOX JELLY FISH amesababisha vifo sio chini ya 5,567 ambavyo vimerokodiwa tangu mwaka 1954, kwani sumu ya mnyama
u huyu huingia zaidi na kushambulia sehemu za moyo (heart attack), mifumo ya neva (nervous systems)
pamoja na tishu za ngozi( skin cells).sumu hii ikimpata kiumbe chochote kwnaza hupata shock(kupararaizi) na kufa haraka mno kwa mshtuko wa moyo.wataalamu wanasema ni vigumu mno kupona labda upate matibabu haraka mno.soma hapa chini jinsi ya kuitibu hiyo sumu kiutaalam zaidi
You have virtually no chance to survive the venomou
 
KING COBRA anashikilia namba mbili kwa wanyama wenye sumu kali mno duniani urefu wake unakadiriwa kuwa ni 5.6 m(18.5ft).mnyama huyu akifanikiwa kukungata mara moja tu huweza kuku ua hapohapo.inasadikika kuwa KING COBRA anaeweza pia kuua tembo(ASIAN ELEPHANT) ndani ya masaa 3 tu.mara nyingi huwa wanapatikana maeneo ya kusini,na kusini mashariki ya ASIA
 
kimuonekano mdudu huyu ni mzuri mno lakini ni miongoni mwa wanyama wenye sumu kali anayeshikilia namba 3 ulimwenguni.wataalamu wanasema kuwa tone moja la sumu ya huyu mnyama linaweza kuua binadamu 20.mazingira wanayopatikana sana ni katika maeneo yenye maji ya chumvi yenye
uvuguvugu na wanashauri kuwa
 
ukifanikiwa kumuona usiwe na wazo hata la kumbeba kwani dhumuni la hiyo sumu ni mawindo(for prey).Dalili za sumu za huyu mnyama zinaweza kuonekana wakati huohuo au unaweza kuchukua muda kidogo kuonekana, na dalili zake kuu huwa ni kupumua kwa shida,unaanza kupata matatizo ya kuona, misuli kupararaizi.hata hivyo mpaka sasa ni vifo30 tu ndivyo vilivyo ripotiwa kutokana na huyu mnyama.
 
BLUE RINGED OCTOPUS ni mnyama ambaye kiumbo ni mdogo mno inasadikika kulingana na umbo la mpira wa golf, sumu yake inasadikika kuwa ni kali mno ambayao inaweza kuua binadamu watu wazima 26 (adult humans) ndani ya dakika moja na hakuna dawa ya kuitibu sumu yake.su
mu yake inapoingia ndani ya mwili wa mtu huwa husikii maumivu(painless) lakini ndani ya muda mdogo tu utasikia uchovu wa misuli,inafuatwa na ukoma na mwishowe ni kufariki.
 
mara nyingi na imezoeleka kuwa ng'e ni wadudu ambao hawazuru kwa binadamu isipokuwa huwa wanaleta madhara madogomadogo kama vile maumivu, ganzi na kuvimba tu. lakini kwa aina hii ya nge ni hatari sana kwani sumu yake ni kali mno ambayo huleta makali na maumivu yake ni vigumu kuyavumilia. kwanza utaanza kusikia homa,kukosa fahamu,kupata degedege,kupararizi na baada ya hapo ni kifo .japokuwa sumu yake ni kali mno ni vigumu kuua kwa mtu mwenye afya nzuri, ila kwa watoto wadogo,wazee, au kwa watu wenye matatizi ya moyo huwa hatari kubwa mno na kuathirika na sumu ya huyu mnyama..
 
Ajira sio salama tena kama ilivyokuwa zamani. Kwa sasa maisha yamekuwa ghali huku kipato cha ajira kikiwa hakitoshelezi. Hii inawafanya waajiriwa wengi kufikiria kuingia kwenye biashara.

Lakini pia kuingia kwenye biashara sio rahisi kama ambavyo mtu anaweza kuona. Kuna changamoto zake nyingi na kama ndio unatokea kwenye ajira huku ukiwa na mahitaji makubwa ya fedha, sio rahisi kuacha ajira na kuingia kwenye biashara moja kwa moja.
 
Biashara ya mtandao(network marketing).
Hii ni biashara ambayo unaweza kuifanya kwa muda mchache kwa siku au kwa wiki na ukaanza kujitengenezea kipato hata kama kwa sasa bado umeajiriwa. Kupitia biashara hii wewe unakuwa msambazaji wa huduma au bidhaa kwa njia ya kuwaambia wengine uzuri wa bidhaa au huduma zile na wanaponunua wewe unapata kamisheni. Kuna faida nyingine nyingi kupitia biashara hii kama kuweza kutengeneza timu kubwa na ikakuongezea kipato kikubwa.
 
Kuwa mkufunzi binafsi.
Kama kuna ujuzi wowote ambao unao, basi jua kuna watu ambao pia wanauhitaji. Wewe unaweza kuwa mkufunzi binafsi kwa ule ujuzi ambao unao. Kwa mfano kama wewe ni mwalimu, basi unaweza kufanya biashara ya kuwa mwalimu binafsi kwa watoto ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia gharama ya juu kidogo. Wewe unakwenda kuwafundisha watoto hao majumbani kwao. Unatoa huduma nzuri na unahakikisha watoto wanaweza kufaulu vizuri.
 
Kama unataka kufanya biashara hii, chagua watoto wa aina gani unataka kufundisha, kisha angalia katika watu unaowafahamu ni wangapi wenye watoto wanaoweza kufaidi huduma zako. Tafuta wachache wa kuanza nao hata kwa gharama za chini, fanya nao kazi vizuri na kama watafurahia waombe wazazi wao wakutambulishe kwa marafiki zao ambao wanaweza kufaidika na huduma unayotoa.
 
Ushauri wa kitaalamu.
Kwa kazi yoyote ambayo unaifanya, wewe una utaalamu fulani. Utaalamu huo unaweza kuwasaidia watu wengi sana ambao hawajui pa kuupata. Kama wewe ni daktari, unaweza kuwa unawapa watu ushauri kuhusu afya zao, wapo wengi sana wanaohitaji ushauri ila hawajui kama unaweza kupatikana, tena kwa bei rafiki kwao. Kama wewe ni mwanasheria uliyeajiriwa, unaweza kuwa unatoa ushauri wa kisheria kama biashara yako ya pembeni.
 
Kama unataka kuingia kwenye biashara hii ya kutoa ushauri wa kitaalamu, jua ule utaalamu ambao unao, kisha angalia ni watu gani wanaweza kunufaika na ushauri wako kisha tafuta wachache wa kuanza nao. Endelea kutoa huduma hii ya ushauri ukilenga kujenga jina na baadae unaweza kutoza gharama au kuongeza gharama kama ulianza na kidogo.
 
Huduma za kitaalamu.
Hii ni tofauti na ushauri wa kitaalamu, hapa unatoa huduma kabisa. Kwa mfano kama wewe ni mhasibu uliyeajiriwa, unaweza kuanzisha biashara yako ya pembeni ya kutoa huduma za kihasibu kwa biashara ndogo ndogo. Wafanyabiashara wengi wadogo hawawezi kumudu gharama kubwa za kupata huduma za uhasibu, kama wewe unaweza kuwaandalia mahesabu yao kwa gharama ambayo wanaweza kuimudu, unaweza kutengeneza biashara kwenye eneo hilo.
 
Back
Top Bottom