Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yeye alikuwa miongoni mwa Waingereza walioendelea kufanya kazi nchini hata pale Tanzania ilipovunja mahusiano yake ya kidiplomasia na Uingereza. Chini ya VSO, utaratibu ulikuwa Wafanyakazi kutoka uingereza walikuwa wanalipwa mshahara ule ule waliokuwa wanalipwa Wafanyakazi wa Tanzania. Mabala ambaye amewahi kufanya kazi kwa muda mrefu mkoani Tabora hupenda kujiita kwa jina la utani la ‘’Mnyamwezi Mkorogo’’.
 
2. TOKA RICHARD SATTERTHWAITE HADI RICHARD MABALA
Alipofika Tanzania, Richard Mabala anasema jina lake la asili lilikuwa ni Richard Satterthwaite ambalo ndilo jina lake tokea kwao. Kutokana na kuwawia vigumu wenyeji kulitamka jina hilo, aliamua kubadili jina na kujiita Mabala. Jina hilo Mabala limetoka wapi? Mwenyewe anasema, “Nilijiunga na kwaya ya Ipuli kule Tabora, mwishoni na baada ya kuzoeana wanakwaya wenzangu walisema kuwa hawawezi kulitamka jina langu na kwamba watanipa la kwao; Mabala. Nilipowauliza lina maana gani wakasema ‘eneo kubwa la nje’ kutoka Uingereza hadi Tabora. Kwa kweli nilianza kulitumia jina hili kwa wasiwasi kidogo nikiona watu wanaweza kuniona najitia kimbelembele kulia kuliko mfiwa, lakini kila mtu akalipenda. Kwa hiyo baada ya kunogewa na kupata uraia nikaliongeza na kuwa jina rasmi”.
 
3. URAIA NA FAHARI YA UTANZANIA
Baada ya kuvutiwa na Tanzania, Mabala alikata shauri kuwa raia kamili wa nchi hii adhwimu. Harakati zake za kusaka Uraia alizianza rasmi mwaka 1979 ambapo Richard Mabala alipeleka maombi ya uraia kwa mamlaka zinazohusika na hilo, maombi yake hayo yakaridhiwa miaka miwili baadaye na akawa Mtanzania kamili. Mabala anasema kuwa hajawahi kamwe kujutia uamuzi wake wa kubadili uraia licha ya kulazimika kupitia mlolongo mrefu wa kuomba Viza kila anapotaka kwenda kumjulia hali mama mzazi yake aliyeko Uingereza.
Mabala anasema kamwe rangi yake haijawahi kuwa kikwazo katika utekelezaji wa shughuli zake mbalimbali hapa nchini.
 
4. MWALIMU WA MA-NGULI
Kwa vipindi tofauti Mabala amefundisha kwenye shule na vyuo mbalimbali nchini. Baadhi ya shule na vyuo alivyofundisha ni Mirambo, Mzumbe, Korogwe, vyuo vya ualimu Chang’ombe na Marangu. Pia amewahi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kati ya mwaka 1973 na 1993. Mabala analikumbuka zaidi darasa lake la kwanza la Shule ya sekondari ya Wavulana Mirambo ambalo lilikuwa na wanafunzi ambao sasa ni wanasiasa na wanazuoni nguli.
Baadhi yao ni Marehemu Profesa Jwani Mwaikusa, Mwanazuoni wa Sheria aliyebobea na Wakili katika Mahakama ya Kimataifa Maalum ya Mashtaka ya Jinai juu ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, ICTR, iliyoko Arusha, Profesa Abdallah Njozi, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro na Mwanafasihi Mbobezi wa Lugha ya Kingereza na Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi.
 
5. MWALIMU MSIKIVU
Baada ya Uhuru, uchapishaji wa vitabu mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili ulishika kasi. Uchapishaji wa vitabu kwa lugha ya Kiingereza hasa vile vya fasihi vilivyoandikwa na waandishi wa kitanzania ulidorora. Kitabu cha ‘’Summons: Poem from Tanzania’’ kilikuwa kati ya diwani za mwanzo kabisa za ushairi wa Kiingereza kuchapishwa nchini baada ya uhuru. Kazi hii ambayo inajumuisha mashairi ya waandishi mbalimbali wa Kitanzania kama Kajubi Mukajanga, Isaac Mruma, Kundi Faraja, Jwani Mwaikusa na Mabala mwenyewe ilikuwa ni zao la ushirikiano wa Mabala na waliokuwa wanafunzi wake wa sekondari. Mabala anasema kuwa wanafunzi wake walikuwa wakimpatia changamoto ya kuandika kazi zake mwenyewe badala ya kuishia kuchambua na kuzikosoa kazi za wengine.
Mabala anasema “Kajubi Mukajanga (ambaye sasa ni Katibu wa Baraza la Habari-MCT) ndiye aliyenishawishi kuandika mashairi wakati yeye alikuwa mwanafunzi na mimi nilikuwa mwalimu wake. Eti kazi yangu ilikuwa kukosoa wengine kwa nini na mimi nisiandike ili nao wapate nafasi ya kunikosoa”.
Mabala aliifanyia kazi rai ya wanafunzi wake na kuandika mashairi na vitabu vingine vya hadithi.
 
6. KUTOKA UHADHIRI HADI MWANAHARAKATI
Baada ya miaka mingi ya ualimu, Mabala aliamua kujikita kwenye harakati za Asasi za Kiraia (AZAKI). Yeye ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa AZAKI maarufu kama Haki Elimu na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na mwishowe kwa kushirikiana na vijana, akaanzisha asasi ya TAMASHA yenye makao makuu jijini Arusha.
Mabala anasema “Nillifundisha Milambo, Mzumbe, Chang’ombe TTC, Marangu TTC, Kibosho Girls na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kisha nikatambua kwamba mimi ni mwanaharakati kuliko mwanataaluma (mhadhiri) ndiyo maana nikaingia AZAKI kwa lengo la kuwawezesha vijana. Nimeanzisha TAMASHA (Taasisi ya Maendeleo Shirikishi) tukihimiza vijana wapate nafasi yao katika jamii”
 
Back
Top Bottom