Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

55281e538fcb08e5cfbc83947dbc0452.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shirikisho la soka nchini Hispania (La Liga) limeliandikia barua shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) wakitoa malalamiko kuhusu ukiukwaji wa sheria za matumizi Financia Fair Play (FFP) unaofanywa na klabu ya Man City.
Raisi wa La Liga Javier Tebas alitoa malalamimo kuhusu wamiliki wa klabu ya Manchester City ambao pia ni wamiliki wa klabu ya PSG kutokana na matumizi makubwa ya kifedha wanayoyafanya.
 
Lakini baadaye shirikisho la soka la UEFA lilitoa majibu kuhusiana na barua iliyoandikwa na Rais wa La Liga kwa kusema kwamba shirikisho hilo halitaichunguza klabu hiyo na taarifa nyingine kinyume na hapo ni uongo.
 
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ''alisita'' wakati wa kutia saini mkataba mpya mwishoni mwa msimu uliopita kwa sababu hakuwa na uhakika kwamba ''angeweza kuiongoza klabu hiyo.''
Wenger alikubali mkataba wa miaka miwili mwezi Mei, mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.
 
Kwenye runinga moja nchini Ufaransa ya Telefoot, alisema alikuwa na ''sababu za kibinafsi'' kutokana na uamuzi uliochelewa wa kuongeza muda wake wa miaka 21 na klabu hiyo.
Arsenal ilimaliza katika nafasi ya tano katika Ligi ya Premia msimu uliopita, ikiwa ni mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nambari nne tangu Wenger alipojiunga na klabu hiyo mwaka 1996.
 
Back
Top Bottom