Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkufunzi wa timu ya taifa Ufaransa Didier Deschamps ameachwa akiwa na ''ghadhabu'' baada ya timu yake kushindwa kuifunga Luxembourg licha ya kupata nafasi nyingi, matokeo yaliyotajwa kuwa ya ''kihistoria'' na mwenzake wa Luxembourg.
Mechi hiyo iliyochezwa Ufaransa ilimalizika kwa sare tasa.
 
Ufaransa ilimiliki mpira katika mchezo huo kwa asilimia 76, na kushambulia mara 34 na kugonga mlingoti wa goli mara mbili lakini hawakufanikiwa kuwafunga Luxembourg kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1914.
''Inaghadhabisha kupata nafasi nyingi hivyo bila kupata goli lolote,'' alisema Deschamps.
 
Kocha wa Luxembourg, Luc Holtz amesema: ''Ni siku ya sherehe kwa soka ya Luxembourg''
Licha ya kucheza na timu iliyoorodheshwa katika nafasi ya 136 ulimwenguni, Deschamps aliwasilisha kikosi kilichojaa wachezaji nyota mechi hiyo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia iliyochezewa Toulouse.
 
90fea025b0fc63eebf2e8768d6cda6e6.jpg
 
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa na kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba na washambuliaji Antoine Griezman wa Atletico Madrid na Kylian Mbappe ambaye amejiunga na PSG hivi majuzi kwa mkopo kutoka Monaco ambapo anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa £166m msimu ujao.
 
Griezmann alipiga kiki kutoka ya umbali wa yadi 30 dakika tano kabla ya wakati wa mapumziko huku Pogba akipata mpira wa mrejesho lakini hakuona lango.
Ingekuwa hatari zaidi kwa Les Bleus, mchezaji wa Luxembourg Gerson Rodrigues alipomzidi Laurent Kosscielny dakika ya 79, lakini kombora lake liligonga mlingoti.
 
Back
Top Bottom