Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dar es Salaam. Kuna msemo usemao, ‘kazi ni kazi bora mkono uende kinywani’.Hata hivyo, baadhi ya watu hujikuta wakifanya kazi ngumu kwa muda mrefu huku wakilalamika siku zote kwa sababu ya kupata fedha.
 
Wanasimulia namna ambavyo wamekuwa wakisafiri kwa shida na wakati mwingine kujikuta wakifungwa pingu kwenye vyuma vya magari yao na askari wa usalama barabarani katika nchi jirani.

Yusuph Mrutu ni mkazi wa Mbezi, Barabara ya Morogoro, ndiye anayefungua mfululizo huu wa simulizi za madereva wa malori na visa wanavyokutana navyo.
 
Nina uzoefu wa muda mrefu wa kuendesha malori, nimefanya kazi hii kwa miaka nane. Mara nyingi safari zetu za kutoka Dar es Salaam kuelekea mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma) huwa zinaanza jioni.

“Wakati mwingine huwa tunakuwa tumepangiwa muda wa kusafiri kwa siku tatu kufika mpakani, lakini mambo hubadilika na safari huchukua muda mrefu zaidi.
 
Mtu unacheleweshwa, wakati mwingine unasimamishwa hata katika vituo ambavyo haustahili kusimamishwa. Ukaguzi unatakiwa uwe unafanyika katika sehemu maalumu, lakini unakuta mtu anakusimamisha mahali ambapo magari hayawezi kupishana,” anasema.

Yusuph anaeleza kuwa wakati wote wanapohangaika kukabiliana na vikwazo wanavyokutana navyo njiani, hufikiria zaidi muda uliopangwa kufika waendako.
 
Taratibu zetu ni kuwa inapofika saa 12:00 jioni unatakiwa kuegesha gari hadi siku inayofuata saa 11:00 asubuhi, lakini inapokugongea saa 12:00 upo Mikumi mbugani inabidi ujisogeze hadi Mikumi mjini maana huwezi kulala pale mbugani,” anasema.

Yusuph anaeleza kuwa mbali na matatizo ya malori kuharibika barabarani au kupata ajali, askari wa barabarani wamekuwa wakiwasumbua kwa kudai rushwa na wanaposhindwa kutoa fedha wakati mwingine hubambikizwa kesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…