Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

c740b7eb4c7066bd5e0e8802ddc4d2f7.jpg
 
[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42]
 
Kwanza tuangalie sababu za makwapa kuwa meusi!
1. Unyoaji…. Wembe unachangia sana kuwa na makwapa meusi…ile puruuu puruuuu aaah mwenzangu lazima kwapa lidate hahahahaaa…. Hapo umetia vijisabuni kidogo unashave kwa nguuuuvu ili kwapa libaki jeupe mpaka mtu nje anaweza uliza jamani kuna usalama uko? anhaaaa!!
 
MISHKAKI YA NYAMA MAHITAJI Nyama 3/4 kg Chumvi kiasi Limau 1 (lemon) Soy souce 1 tbsp Bizari nzima (cumin seeds) 1tbsp Pilipili manga (black paper) 1/2 tsp Tangawizi 1tsp (ginger paste) Kitinguu saum 1tsp (garlic paste) Mafuta ya kupikia 2tbsp Pilipili ilosagwa (ukipenda) JINSI YA KUTENGENEZA Weka bizari nzima kwenye pan weka kwenye moto ikipata moto kidogo itowe uitwange Changanya vitu vyote pamoja than weka chops Funika weka kwa masaa 4 ikolee vizuri Chomeka nyama kwenye vijiti Weka kwenye trayer tia kwenye grill igeuze geuze kila wakati ili iwive vizuri
 
VEGETABLE FRIED RICE MAHITAJI Mchele 1/2 kg Mix vagetable 1 cup Chumvi kiasi Mafuta 3 tbsp Soy source kiasi Kitunguu maji 1 cha kiasi (kikate kama cha sambusa) Kitunguu saumu tembe 1 JINSI YA KUTENGENEZA Kwanza chemsha wali wako kama kawaida uwive lakini usivurugike ukisha kuuchuja maji uweke pembeni Kwenye sufuria ya kupikia weka mafuta 3 tbsp weka kitunguu maji changanya mpk kilainike kisipige rangi weka kitunguu saumu iloparwa changanya vizuri Sasa weka mix vegetable zako changanya na vitunguu maji mpaka vikaangike weka chumvi kidoogo Sasa weka wali wako ulochemsha mwagia juu soy source changanya vizuuri na wali wako utakuwa tayari kwa kuliwa ENJOY
 
MAANDAZI YA CUSTARD MAHITAJI unga wa ngano 1/2 kg Hamira 2 tsp Sukari 100 gm Maziwa ya maji 100ml Chumvi 1/2 tsp Maji 1/2 kikombe Yai 1 Butter 100gm Unga wa Custard 2tblsp Mafuta ya kupikia MATAYARISHO Changanya unga wa ngano, unga wa custard, hamira (hamira unaweza kuiroweka kabla ya kuchanganya) chumvi, sukari na butter pamoja mpaka ichanganike vizuri. Piga yai na maziwa pamoja mpaka yai lichanganyike na maziwa. Halafu tia kwenye unga changanya. Tia maji kidogo kidogo mpaka uwe donge laini. Si lazima utumie maji yote na kama kidogo ongeza. Ukande unga kwa dakika 15. Ufunike uwache uumuke. Ukiwa tayari kata size unopenda. Yaweke tena yaumuke. Halafu choma kwa mafuta. Yakiiva yachuje mafuta yaache yapowe. Ukipenda saga sukari unyunyize juu yake. Tayari kwa kuliwa na chai ya maziwa.
 
MAANDAZI YA KAWAIDA MAANDAZI YA NAZI MAHITAJI unga vikombe (mug) 2 Sukari robo kikombe (ongeza kama unapenda) Tui la nazi kikombe kasoro Hiliki 1tsp Hamira 2 tsp Mafuta ya kupikia (kwa ajili ya kuchomea) MATAYARISHO Chekecha unga uwe msafi, changanya na sukari, hiliki na hamira. Tia tui la nazi kidogo kidogo mpaka ushikane. Si lazima utumie tui lote tizama kiasi ya kuwa unga unaweza kukandika bila matatizo. Kanda unga mpaka uwe laini, ufunike uwache kwa dakika 10. Halafu Ukande tena kwa dakika 2-3. Fanya madonge yaliyokuwa sawa sawa kwa size. Sukuma kila donge kama chapati lakini usiwe mwembamba sana. Kata sehemu nne. Weka unga mkavu kwenye tray yaweke maandazi juu yake, wacha yaumuke (muda wa kuumuka inategemea na hamira unotumia). Yakisha kuumuka weka mafuta kwenye jiko kwa moto wa kati yakishakupata moto tia andazi moja moja usitie mengi acha nafasi ya kuyageuza. Ukishakuyatia tu usiwache mpaka yakaiva upande mmoja yageuze kila wakati ili yawive sawasawa pande zote mbili bila kufanya mstari mweupe. KUMBUKA MOTO UKIWA MKUBWA YATAIVA NJE NDANI YATAKUWA MABICH. MOTO UKIWA MDOGO SANA YATAINGIA MAFUTA NDANI. Yakiiva ENJOY
 
CAKE MAHITAJI Siagi/butter 1 cup Sukari 1cup (sukari ilosagwa) Unga wa ngano 1 1/3 cup Mayai 5 Condenced milk 4 tbsp Baking powder 1 1/2 tsp Arki/vanilla kijiko 1 Cocoa 2 tsp (unaweza kueka rangi) Unga wa maziwa (nido) 2 tbsp (ukipenda) MATAYARISHO: Saga siagi na sukari kwa mashine (hand mixer) mpaka ilainike iwe kama cream (about 10mins) , tia mayai uendelee kusaga kidogo ,weka condenced milk na b.powder na arki saga kidogo than weka unga wako na nido saga tena mpaka uchanganyike vizuri Weka vijiko vitano (tbsp) vya mchanganyiko kwenye kibakuli kidogo weka na cocoa changanya kwa mashine kidogo Chukua treya paka siagi chini ili keki isigande weka half mchanganyiko mweupe weka mchanganyiko wenye cocoa than malizia ule mweupe ulobaki Weka katika oven choma kwa medium heat (160°) kwa 30mins (au iangalie mpaka utie kijiti kati kitoke kikavu) Note: Inaweza kuchukua muda zaidi kuchoma kama utaichoma kwenye treya ndogo kama hutaki kueka maziwa (condenced milk) unaweza ku substitute kwa kuongeza yai moja ENJOY
 
FRUITS ICE LOLLY MAHITAJI Strawberry kiasi Mango (embe mbivu ) kiasi Sukari kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Saga strawberry zako kwa blender weka kwenye kibakuli weka sukari kiasi unayopenda changanya vizuri kama hupendi kuweka sukari sio lazima Anza kuweka kwenye vikopo vyako kila kikopo nusu than weka kwa frizer kwa muda wa saa moja au hata zaid sio mbaya Baadae toa saga embe lako kwa blender jalizia kwenye vikopo vyako nafasi ilobaki chomeka vijiti vyako weka kwenye frizer mpk zigande tayari kwa kuliwa ENJOY (UNAWEZA KUTUMIA FRUITS UNAZOPENDA )
 
VIAZI /POTETOES / VIAZI ULAYA/ VIAZI MVIRINGO VYA NAZI MAHITAJI Viazi1/2kg Kitunguu thaum 1tsp Kitunguu maji 2 (chopped) Nyanya (tomatoes) 3 kubwa ( chopped) Tui la nazi 2 vikombe Limau moja Bizari ya njano 1tsp Pilipili nyekundu ukipenda Chumvi kiasi Mfuta ya kupikia 2tblsp Coriander leaves kwa kupambua sio lazima. MATAYARISHO Chemsha viazi mpaka viive menya maganda kata size unopenda weka pembeni. Kaanga vitunguu maji na thom mpaka viwe laini tia bizari na nyanya kaanga mpaka ziive vizuri na nyanya zilainike. Tia tui acha lichemke kwa dakika kama 5 tia ndim, chumvi na pilipili. Halafu weka viazi kwenye tui linalochemka, acha kwa dakika 2 kwenye jiko. Onja kama kila kitu kiko sawa. Tayari kwa kuliwa ENJOY Kula kwa wali, mikate ya aina zote au kula tu peke yake.
 
Back
Top Bottom