Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

CHOCOLATE CAKE MAHITAJI Unga 2 cups Sukari 1 3/4 cup ( nimetumia icing sugar) Cocoa powder 3 tbsp Drinking chocolate powder 4 tbsp Baking powder 1 tbsp Mayai 5 Siagi 1 cup Maziwa 1 1/4 cup Vanila 1 tbsp ( unaweza kutumia esse JINSI YA KUTENGENEZA Kwanza washa oven lako moto 180 Changanya unga , baking powder , cocoa powder na chocolate drinking powder vizuri weka pembeni Kwenye bakuli la kusagia cake weka siagi na sukari saga kwa mashine mpk iwe cream weka yai moja moja huku unasaga kwa mashine (HAPA HAKIKISHA UNASAGA SANA ILI CAKE YAKO ISIWE NA HARUFU YA MAYAI) Sasa weka unga na maziwa kwa matabaka matatu ( NAKUSUDIA ANZA KUWEKA MAZIWA KIDOGO THAN UNGA KIDOGO, MAZIWA UNGA, MAZIWA TENA MALIZIA NA UNGA ) kila ukiweka uwe unachanganya kwa mashine yako weka vanila yako Baadae paka siagi treya yako ya kuchomea mimina mchanganyiko wako weka kwenye oven kwa muda wa dakika 30 mpka 40 au mpk iwive ENJOY
 
NYAMA YA KUCHOMA (GRILLED CHOPS) MAHITAJI Chops vipande 10 (10 pieces) Chumvi kiasi Limau 1 (lemon) Soy souce 1 tbsp Bizari nzima (cumin seeds) 1tbsp Pilipili manga (black paper) 1/2 tsp Tangawizi 1tsp (ginger paste) Kitinguu saum 1tsp (garlic paste) Mafuta ya kupikia 2tbsp Pilipili ilosagwa (ukipenda) JINSI YA KUTENGENEZA Weka bizari nzima kwenye pan weka kwenye moto ikipata moto kidogo itowe uitwange Changanya vitu vyote pamoja than weka chops Funika weka kwa masaa 4 ikolee vizuri Weka kwenye trayer tia kwenye grill mpaka iwive uigeuze pande zote mbili Enjoy
 
MANGO LASSI MAHITAJI Mango pulp 1 cup Mtindi (natural yorgut) 1 cup Maziwa (milk) 1/2cup Sukari (sugar) 3 tbls Hiliki (cardamon powder)1/4 tsp JINSI YA KUTENGENEZA Weka vitu vyote kwenye blender saga mpaka vichanganyike Unaweza kuongeza sukari kwa testy yako weka barafu au weka kwenye fridge ipate baridi Nzuri sana utajiramba Enjoy Mango pulp ni embe ilosagwa nzito so kama huna unaweza kutengeneza kwa embe ilowiva vizuri iwe haina manyuzi unatowa maganda than unasaga kwa blender
 
PILAU YA NYAMA MAHITAJI Mchele 2 cups Nyama 1/2 kg (nimetumia kondoo unaweza kutumia yoyote) Vitunguu maji 3 medium (chopped) Mbatata(potatoes) 2 Mdalasini mzima 3 Hiliki nzima 5 Hiliki ya unga 1/4 tsp Pilipili manga nzima 1/2 tsp Bizari nzima 1/2 tsp Mafuta ya kupikia 1/3 cups Tangawizi 1/2 tsp Kitunguu saumu(garlic) 1/2 tsp Chumvi kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Ikate nyama kosha ichemshe na tangawizi, garlic, chumvi na bizari nzima kidogo, ikiwiva weka pembeni ibakishe na soup kwa ajili ya kupikia wali Kosha mchele uroweke kwa 1hr Kaanga vitunguu vikianza kupiga rangi weka mdalasini,hiliki, bizari nzima, pilipili manga kaanga kidogo than tia mbatata zikaange kidogo than tia nyama uwache kidogo ijikaange ,tia soup ikianza kuchemka tia mchele(hakikisha soup iwe imeufunika mchele na kuzidi kidogo) kama soup haijatosha unaweza kuongeza maji ya moto Onja chumvi , weka moto wa kati wacha uchemke uwe unaukoroga usigande mpaka ukikauka(usikauke sanaa) weka kwenye oven ENJOY NA SALAD OF UR CHOICE
 
MCHUZI WA PWEZA WA NAZI MAHITAJI Pweza mmoja mdogo(kama mkubwa nusu) Tungule/nyanya(tomato) 1 chopped Kitunguu maji 1 Mbatata(potatoes) 3 zikate Carrot 1 Pilipili hoho (mix pappers) 1/2 Tui la nazi (coconut milk) kiasi Mafuta 5tbsp Bizari manjano 1/2 tsp Bizari nzima (cummin powder) 1/2tsp Chumvi kiasi Tangawizi 1/2 tsp Kitunguu saum (garlic paste) 1/2 tsp Ndimu (lemon juice) 2 tbsp kitmiri(corriander leaves) kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Mkate pweza mkoshe mueka garlic ,tangawizi ,chumvi na cummin powder mchemshe akikaribia kuiva weka mbatata chemsha pamoja mpaka ziwive na zikauke maji yote Kwenye pan weka mafuta kaanga vitunguu mpaka vikilainika tia carrot na mix pappers kaanga kidogo than weka tungule mpaka zilainike weka bizari ya manjano than mtie pweza na mbatata changanya vizuri weka tui la nazi (kiasi cha kufunika pweza au kiasi unachotaka uchuzi wako uwe) wacha vichemke kidogo tia ndimu than test size yako ya chumvi (usiache ukauke sana coz ukipoa utazidi kukauka) Ukimaliza tia corriander Enjoy na mikate ,wali au chochote
 
JUICE MAHITAJI EMBE MBIVU 1 NANASI 1 NDIZI MBIVU 2 TANGAWIZI KIASI SUKARI KIASI MAJI MATAYARISHO saga fruits zote na tangawizi kwenye blender (usisahau kuvimenya). Halafu Weka kwenye bakuli kubwa, tia maji na sukari. Mix vizuri onja sukari kama iko sawa. Ichuje tia barafu tayari kwa kunywa. Ni tam sana
 
PILAU YA NYAMA MAHITAJI Mchele 2 cups Nyama 1/2 kg (nimetumia kondoo unaweza kutumia yoyote) Vitunguu maji 3 medium (chopped) Mbatata(potatoes) 2 Mdalasini mzima 3 Hiliki nzima 5 Hiliki ya unga 1/4 tsp Pilipili manga nzima 1/2 tsp Bizari nzima 1/2 tsp Mafuta ya kupikia 1/3 cups Tangawizi 1/2 tsp Kitunguu saumu(garlic) 1/2 tsp Chumvi kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Ikate nyama kosha ichemshe na tangawizi, garlic, chumvi na bizari nzima kidogo, ikiwiva weka pembeni ibakishe na soup kwa ajili ya kupikia wali Kosha mchele uroweke kwa 1hr Kaanga vitunguu vikianza kupiga rangi weka mdalasini,hiliki, bizari nzima, pilipili manga kaanga kidogo than tia mbatata zikaange kidogo than tia nyama uwache kidogo ijikaange ,tia soup ikianza kuchemka tia mchele(hakikisha soup iwe imeufunika mchele na kuzidi kidogo) kama soup haijatosha unaweza kuongeza maji ya moto Onja chumvi , weka moto wa kati wacha uchemke uwe unaukoroga usigande mpaka ukikauka(usikauke sanaa) weka kwenye oven ENJOY NA SALAD OF UR CHOICE
 
CHAPATI MAHITAJI Unga wa ngano vikombe 2 Samli (kimbo) nusu kikombe ( kila kikombe kimoja cha unga, pima samli iliyoyayushwa robo ya kile kikombe). Kama unga vikombe 2 samli nusu kikombe. Chumvi kiasi. Sukari kijiko kimoja cha chai. (Inafanya chapati ziwe laini). MATAYARISHO: Changanya samli, unga sukari na chumvi pamoja mpaka uchanganyike vizuri. Tia maji ya moto yasiwe yamoto sana ili uweze kukanda. Changanya uwe donge ukiona mkavu ongeza maji ya moto. Kanda mpaka uwe laini uone kama unavutika ukiuvuta usiwe unakatika kama unakatika basi ongeza maji kidogo . Ukiona upo tayari ufunike fanya kazi zako kwa dakika 20 - 30. Kata madonge paka samli iloyayushwa utakapoweka madonge (inasaidia wakati wa kukanda yanakuwa laini hutumii nguvu). BaadaYa kupumzika chukuwa donge moja moja litandaze mpaka liwe transparent. Halafu unapaka samli iloyayushwa unanyunyiza na unga mkavu juu. (Unga unasaidia zikisha kupikwa zinakuwa zinavutika) Unageuza upande wa pili unafanya same thing. Unakunja kama plits. Unazungusha duara unaziacha kwa dakika 10 unakanda chapati unachoma na samli.
 
```MC ANAMSIFIA BI HARUSI

Sasa nawapa sifa kubwa ya Bibi Harusi wetu huyu. Pamoja na kupendeza saana. Tangu namfahamu huwa havai nguo za ndani. Watu wote ukumbini wakaduwaa! Bw. Harusi macho yakamtoka, Bi harusi akaanza kutetemeka.

MC-Narudia tena kwa msisitizo na sijakosea. Bi Harusi huyu havai kabisa nguo za ndani. Yeye anavaa za nje ya nchi tu, kutoka Italy, England na USA si za Tanzania. Hebu mshangilieni."

Kila mtu "Ahaaaa kuuumbe!!!"

Je, asingefafanua ingekuwaje?```
 
SPICE CHIPS MAHITAJI Viazi potetoes 2 Pilipili manga 1tsp Bizari njano 1/2 tsp Paprika au bizari nyekundu 1 tsp Pilipili ya unga 1/2tsp Mafuta ya kupikia 4 tblsp Ufuta 2tsp Tanduri masala 1 tsp Chumvi kiasi Rojo la ukwaju 3 tblsp MATAYARISHO Kata viazi design ya chips lakini ziwe nyembamba ili zisichelewe kuiva. Zikoshe uzichuje maji. Tia mafuta kwenye dish weka kwenye jiko, moto mdogo mdogo.Halafu tia ufuta, pilipili manga, bizari, tandoori na paprika kaanga kwa sekunde 30 halafu tia chips changanya vizuri halafu endelea kuzigeuza mpaka ziive (ukichanganya uwe gently usizikate). Zikisha kuiva tia chumvi pilipili na ukwaju, mix kwa dakika kidogo onja kama kila kitu kiko sawa tayari kwa kuliwa. ENJOY
 
SANDWICH MAHITAJI Sles za mkate 4 Yai 1 Bread crumb kiasi Pilipili ya kuwasha 1/2 (kipande) Chumvi kidogo sana Nyama ya salami vipande 4 Mafuta ya kuchomea kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Chukua sles zako za mkate kata ile nyama ya kati kwa kutumia donuts cuter au hata glass utapata shape kama pict ya mwanzo hapo juu weka pembeni Chukua moja weka vipande viwili vya salami na pili pili juu kama pict no 2 than chukua kipande chengine cha sles ya mkate funika juu yake Weka mafuta yako kwenye karai yapate moto vizuri chovya sandwich yako kwenye yai ulolipiga na chumvi kidogo ukiitoa kwenye yai ibane bane pembeni kidogo Baadae garagiza kwenye bread crumb choma kwenye mafuta (deep fry) huku unageuza mpk ipige rangi vizuri fanya na ilobaki hivo hivo Tayari kwa kuliwa ENJOY NI YUUMMY
 
Back
Top Bottom