PILAU YA NYAMA MAHITAJI Mchele 2 cups Nyama 1/2 kg (nimetumia kondoo unaweza kutumia yoyote) Vitunguu maji 3 medium (chopped) Mbatata(potatoes) 2 Mdalasini mzima 3 Hiliki nzima 5 Hiliki ya unga 1/4 tsp Pilipili manga nzima 1/2 tsp Bizari nzima 1/2 tsp Mafuta ya kupikia 1/3 cups Tangawizi 1/2 tsp Kitunguu saumu(garlic) 1/2 tsp Chumvi kiasi JINSI YA KUTENGENEZA Ikate nyama kosha ichemshe na tangawizi, garlic, chumvi na bizari nzima kidogo, ikiwiva weka pembeni ibakishe na soup kwa ajili ya kupikia wali Kosha mchele uroweke kwa 1hr Kaanga vitunguu vikianza kupiga rangi weka mdalasini,hiliki, bizari nzima, pilipili manga kaanga kidogo than tia mbatata zikaange kidogo than tia nyama uwache kidogo ijikaange ,tia soup ikianza kuchemka tia mchele(hakikisha soup iwe imeufunika mchele na kuzidi kidogo) kama soup haijatosha unaweza kuongeza maji ya moto Onja chumvi , weka moto wa kati wacha uchemke uwe unaukoroga usigande mpaka ukikauka(usikauke sanaa) weka kwenye oven ENJOY NA SALAD OF UR CHOICE