MAPISHI YA MAANDAZI YA MITAI (MAANDAZI YA SUKARI JUU|SHIRA)
MAHITAJI
Unga wa ngano
Baking powder Kijiko cha chai kimoja
Baking soda ¼ Kijiko cha chai
Kungumanga(nutmeg) kijiko cha chai 1/2
Chumvi kijiko cha chai
Sukari 1 kijiko cha chakula
Hamira 1/2 Kijiko cha chakula
Yai moja
Maziwa ½ Kikombe
Mafuta ya kukaangia
SHIRA
Sukari Kikombe komoja
Maji ½ Kikombe
Iliki au Mdalasini kiasi iliosagwa
NAMNA YA KUANDAA
Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari, kungumanga na hamira.
Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.
Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga; na ukande kama unga wa maandazi.
Kisha weka katika bakuli la ufiniko na uache mchanganyiko wako uumuke.
Unga ukishaumuka , sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai.
Bandika fying pan yakishapata moto mafuta na kaanga hadi yawe rangi ya brown kiasi
Ipikie shirakwa kuichemsha lakini isiwe nzito.
Mimina mitai na upepete acha ipoe na kukauka itakuwa tayari kuliwa / pia shira waweza kufanya ile ya kioo ukipenda