Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aidha, Pale unapo ona njia mbili za awali huna, nabado una mahitaji ya mtandao unaweza kutumia “Hotspot” inayopatikana katika eneo husika ila, Hakikisha haikuhitaji uingize taarifa zako binafsi kabla ya kuanza kupata mtandao na pia ujenge tabia ya kuhakiki kama ni sahihi ambapo unaweza hata kuuliza tu kwa mhudumu kama unayopaikana/ iona kweli ni ya kwao.
 
Vipimo:
Karanga - Kilo
Sukari - 5 vikombe
Maji - 2 vikombe
Maziwa ya unga - 2 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.
Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.
Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.
Paka mafuta treya kisha mimina na utandaze upesi upesi.
Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.
Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.
 
Vipimo:
Karanga - Kilo
Sukari - 5 vikombe
Maji - 2 vikombe
Maziwa ya unga - 2 vijiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:
Saga karanga zilizokaangwa na kumenywa mpaka zilainike kiasi.
Kisha changanya maji na sukari weka jikoni yachemke mpaka yanate kidogo kama shira. Changanya unga wa karanga na maziwa ya unga kisha mimina kwenye hiyo shira.
Koroga taratibu kwa moto mdogo mpaka uone imeshikana na inanata.
Paka mafuta treya kisha mimina na utandaze upesi upesi.
Acha ipoe kidogo tu kisha katakata vipande na acha ipoe kabisa.
Panga kwenye sahani tayari kwa kuliwa pamoja na kahawa.
Kidokezo:
Kama maziwa ya unga huna si lazima.
 
SOMA NAMNA YA KUTUMIA TANGAWIZI KWA TIBA
Tangawizi hutibu kutokusagika kwa chakula tumboni, Gesi tumboni, Msokoto wa tumbo (bila kuharisha), Kutapika, Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.
 
1. KWA KUVIMBIWA NA KUTAKA HAMU YA KULA.
Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula. Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.
 
2. MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.
3. KWA KUHARISHA
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.
4. KWA KISUKARI
Kunywa Juice ya Tangawizi iliyochanganywa na Sukari mawe.
5. KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.
 
6. MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI
Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.
7. MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.
8. KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA
Chukua Tangawizi ya Unga na uweke
 
JUICE YA CARROT NA MACHUNGWA :
Mahitaji :
Karoti 2 kubwa zilokatwa vipande
Nanasi ilokatwa vipande vikombe 2
Machungwa yalomenywa 2
Asali au sukari kiasi
Chumvi kidogo
Recipe :
Anza kwa kuandaa mahitaji kwa kumenya na kuvikata kata
Weka mahitaji kwenye blenda na usage mpaka ilainike. Ongeza maji kiasi kupata juice kutoka kwenye makapi kapi
Chuja kisha tia sukari au asali na chumvi. Mimina kwenye glasi pamoja na barafu na andaa kuinywa
 
MAPISHI YA MAANDAZI YA MITAI (MAANDAZI YA SUKARI JUU|SHIRA)
MAHITAJI
Unga wa ngano
Baking powder Kijiko cha chai kimoja
Baking soda ¼ Kijiko cha chai
Kungumanga(nutmeg) kijiko cha chai 1/2
Chumvi kijiko cha chai
Sukari 1 kijiko cha chakula
Hamira 1/2 Kijiko cha chakula
Yai moja
Maziwa ½ Kikombe
Mafuta ya kukaangia
SHIRA
Sukari Kikombe komoja
Maji ½ Kikombe
Iliki au Mdalasini kiasi iliosagwa
NAMNA YA KUANDAA
Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari, kungumanga na hamira.
Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.
Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga; na ukande kama unga wa maandazi.
Kisha weka katika bakuli la ufiniko na uache mchanganyiko wako uumuke.
Unga ukishaumuka , sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai.
Bandika fying pan yakishapata moto mafuta na kaanga hadi yawe rangi ya brown kiasi
Ipikie shirakwa kuichemsha lakini isiwe nzito.
Mimina mitai na upepete acha ipoe na kukauka itakuwa tayari kuliwa / pia shira waweza kufanya ile ya kioo ukipenda
 
BARFI ZA MAPERA
Njugu robo kilo zisage mapande mapande Maziwa ya unga kikombe kimoja Unga wa ngano kikombe kimoja Sukari kikombe kimoja n nusu Maji kikombe kimoja Rangi nyekundu kiasi
Teleka maji . Tia sukari n rang mpka shira inate. Tia njugu koroga.tia unga n maziwa koroga .epua wacha ipowe fany madonge . sukari kikombe kimoja n nusu .maji kikombe kimoja . Unga wa ngano kikombe kimoja .rang ya kijan .teleka maji na sukari na rangi mpaka shira inate .wacha ipoe .chota mchanganyiko wa kijan uuvishie donge jekundu kama unafany egg chop .ukimaliza chukua karafuu ichomeeke juu ya pera .
 
BADIA ZA MUHOGO MBICHI
Mahitaji
Muhogo mbichi kiasi unachotaka
Nazi iliyokuwa haijachujwa
Vitunguu maji na thoum kiasi
Pili pili za kuwasha
Chumvi kiasi
Mafuta kwa ajili ya KUCHOMEA
Unasaga muhogo baadae unaukamuwa maji yake unachukua nazi unaichanganya na muhogo nabizari ya manjano unautwanga kwenye kinu halafu unautoa unachanganya na vitu vilivyobaki unafanya badia zako baadae unazichoma kwa mafuta tayari kwa kula
kuchomea
 
PERA MAZIWA
Vipimo
Maziwa ya unga 2 vikombe
Sukari 3 vikombe
Maji 3 vikombe
Unga wa ngano ½ kikombe
Mafuta ½ kikombe
Iliki kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Paka sinia mafuta kabla ya kupika pera maziwa
Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
NB za rangi unaweka food colour wakati ukiweka mchanyiko wa sukari
 
[emoji39] [emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Chachandu ya carrot na ukwaju
Mahitaji
-carrot mbili kubwa
-ukwaju unakisia
-Pili Pili mbichi kisia kulingana na mapenzi yako
-chumvi kdgo kisia
Jinsi ya kuandaa
-loweka ukwaju kwenye bakuli na maji kiasi (maji kisia yatakayoweza kuivisha carrot zako)
-menya carrot katakata vipande vikubwa vikubwa weka kwenye sufuria
-kata kata pilipili changanya kwenye carrot zako
-sugua ukwaju ulio uloweka upate juice nzito nzito ,chuja na chujio ili kuondoa nyuzinyuzi za ukwaju kisha mimina kwenye carrot zako
- weka chumvi kdgo kisha chemsha mpaka carrot ziive,zisiive sana mpaka kulegea
- carrot zikisha iva,acha zipoe kabisa,kisha mimina kwenye blender na usage, chachandu yako itakua tayari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…