Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nilisoma shule za masista,kule ukivaa mkufu ukakamatwa kama hauna msalaba utapata adhabu kubwa ila mkufu ukiwa na msalaba hawakufanyi chochote. Ndio ishu ya Lissu imegeuzwa hivyo,yaan from nowhere mtu anakuja na topic ya lissu anapokelewa kwa mikono miwili na discussion inaanza. ila kipindi kile mzima wa afya, watu walijitahidi kuzipotezea topic zake zikiletwa humu wanaambiwa wapeleke jukwaa la siasa
Asante Numbisa. Binadamu unafiki mtupu!!!
 
Watu wengi wanaugua magonjwa ya tumbo lakini ni wachache wanaofahamu kuhusu ugonjwa wa amoeba unaosababishwa na uchafu wa mazingira, vyombo vya nyumbani ambao huenezwa kupitia bakteria anayejulikana kama Entamoeba histolytica.
Vimelea vinavyoenezwa na bakteria huyu humsababishia mtu kuhara haja ambayo huonekana ina kamasi.
 
Ulaji wa matunda bila kuyaosha au kutokunawa mikono baada ya kutoka chooni, kula chakula bila kunawa mikono na kunywa maji yasiyochemshwa zinaelezwa kuwa ni baadhi ya namna zinazosaidia kuwasambaza bakteria hawa hivyo kuenea ugonjwa huu.
Mgonjwa hupata maambukizi baada ya kunywa au kula kitu kilichochanganyika na Entamoeba histolytica ambao hukimbilia kwenye utumbo mdogo ambako huzaliana. Wakiwa wengi, huenda kwenye utumbo mkubwa na kuanza kushambulia mwili.
 
Wakikua, huishi katika kinyesi cha binadamu kisha hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kuishi katika ardhi kwa muda wa wiki nne, kipindi ambacho huwa na uwezo wa kusababisha maambukizi kwa yeyote atayekutana nao. Wanaweza kusambazwa kwa kutokunawa mikono vizuri baada ya kujisaidia, kusambazwa na nzi, kusafisha vyombo kwa maji yasiyo salama au kushikana mikono na mtu mwenye bakteria hao.
 
Wakikua, huishi katika kinyesi cha binadamu kisha hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kuishi katika ardhi kwa muda wa wiki nne, kipindi ambacho huwa na uwezo wa kusababisha maambukizi kwa yeyote atayekutana nao. Wanaweza kusambazwa kwa kutokunawa mikono vizuri baada ya kujisaidia, kusambazwa na nzi, kusafisha vyombo kwa maji yasiyo salama au kushikana mikono na mtu mwenye bakteria hao.
 
Kati ya watu milioni 40 mpaka 50 duniani kote wanasemwa kuugua ugonjwa huu ambao husababisha vifo 100,000 kila mwaka. Mara nyingi, waathirika wengi huwa hawafahamu kama wanaugua maradhi haya hivyo kuchelewa kupata matibabu stahiki.
Walio kwenye hatari
Jamii inayoishi katika mazingira yasiyokuwa na maji salama ipo kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa amoeba kwani huchota maji kutoka kwenye mito kwa matumizi ya nyumbani bila kujali kwamba hayakidhi vigezo vya kiafya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…