Jambo la pili
Tai wanauwezo wa kuona mbali sana. Wanaweza kuona kitu kilichoko umbali wa kilometa tano. Tai akiona mawindo yake huangalia pale pale na huanza kwenda kukamata mawindo hayo kwa kasi kubwa. Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.
Tunajifunza nini? Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame maono yako bila kuangalia pembeni mpaka uyapate au uyatimize hiyo ndiyo siri ya kuelekea mafanikio yako, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe kaza mwendo bila kurudi nyuma.