Inakadiriwa kuwa mnyama huyo huishi kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika pori. Lakini hiyo ilikuwa inafahamika zamani kipindi ambacho mnyama huyo alikuwa anaonekana tofauti na sasa.
Hata hivyo, kutokana na aina ya maisha ya wanayoishi, inasemekana kuwa wanaweza wasiishi miaka mingi, licha ya kuwa bado haifahamiki kwa sasa, inawezekana wakaishi kwa miaka 20.
Inakadiriwa kuwa kakakuona 100,000 hukamatwa kila mwaka barani Afrika na Ulaya na kuuzwa. China na Vietnam ndizo nchi maarufu ambazo nyama na magamba yake huuzwa.
Kutokana na hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hifadhi za Asili (IUCN) limemweka kakakuona kwenye orodha ya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka duniani.