Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ulimi mrefu kuliko mwili wake

Kakakuona ana ulimi wenye urefu unaozidi mwili wake. Akiurefusha kwa kuutoa nje ya kinywa unafikia urefu wa sentimita 40.

Ulimi huo ambao pia unanata, huutumia kwa ajili ya kukusanya wadudu ambao ndiyo mlo wake wa pekee, hana mwingine zaidi ya huo kutokana na kukosa meno.
 
Ndiye mnyama pekee duniani ambaye mwili wake wote umefunikwa na magamba makubwa

Magamba yanayofunika mwili wa mnyama huyo ni makubwa kuliko ya viumbe wengine. Magamba hayo kitaalamu yameundwa na kitu ninachoitwa ‘keratin’, ambayo yanafanana na yale yanayounda kucha za binadamu.
 
550cf62de04ec7417fe094846bf43904.jpg
 
Maana ya jina kakakuona

Maana ya jina hilo ilianzia nchini Malaysia, Indonesia na Brunei likimaanisha kitu kinachojikunja. Kakakuona hupenda kujikunja kama mpira. Hiyo ikiwa kama mbinu anayotumia kujilinda dhidi ya maadui.

Licha ya kuwa hutumia mbinu hiyo kujilinda, lakini anapojikunja ndiyo inakuwa rahisi kwa watu kumkamata na kumbeba.
 
Huishi juu ya miti

na katika mashimo

Baadhi ya kakakuona huishi juu ya miti, wengine hujichimbia ardhini na kuishi ndani ya mashimo.

Wengi wanaoishi juu ya miti ni wale wenye mikia mirefu wanaopatikana barani Afrika. Wengine huchimba mashimo marefu ardhini na kuishi humo ili wasikutane na binadamu.
 
Si rahisi kushambuliwa

na wanyama wengine

Ukiachilia mbali adui yao mkubwa ambaye ni binadamu, adui wengine wa wanyama huyo ni jamii ya chui na simba.

Hata hivyo, maadui hao hushindwa kuwashambulia kakakuona kutokana na namna wanavyojilinda kwa kujikunja na jinsi mwili wao ulivyo na magamba. Kutokana na hali, hiyo inakuwa vigumu kwa simba au wanyama wengine kuwashambulia kwa kuwala.
 
Back
Top Bottom