Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

lakini fisi ni mnyama anayewinda na hula nyama fresh, akikosa mawindo yake hufanya uporaji kwa wanyama kama simba na inapokosekana hata nafasi hiyo, basi akikutana na mfupa,mzoga yeye hana neno. Wakati wanyama wengine wengi wakiwa wanaongozwa na madume, ukifika katika koo za fisi majike ndio viongozi, lakini mbali na uongozi pia fisi jike ana nguvu za mwili kuliko dume,
 
bahati waliyonayo mbaya wanyama hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike lijifunguapo, watoto wao wengi hufa wakati mama yao anapozaa, hivyo kama jike atazaa wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.
 
SIFA ZAKE ZA KIPEKEE***************************** Mosi ni mnyama mnyonge lakini huweza kupola chakula kwa wanyama wakali kama simba. Fisi ni mnyama anayeweza kukimbia umbali mrefu kwa taratibu, we tangulia na spidi 120 yeye atakuja na 30 na atakukuta tuu njiani ukiwa umeanguka either kwa kuishiwa nguvu au misuli kukaza na hapo ndio atafanya biashara yake kwa urahisi, na sifa hii ndio watu husema eti anasubiri mtu adondoshe mkono wala sio kweli, ana akili zake.
 
Fisi huzaliwa akiwa macho ujue. Fisi jike huwa na maamuzi yote kuanzia mahabani mpaka mgawanyo wa kazi. Fisi dume ni mnyama bwege anatawaliwa na jike lake. Fisi ni kiumbe asiye na mbio za kasi. Fisi hunguruma, hucheka pia hutoa milio mbali mbali inategemea na alipo, na hiyo huwa ni lugha wanayotumia kuwasiliana akifanya hivyo wenzie wakisikia wanajua tuu kuna jambo gani limemsibu mwenzao.
 
Fisi jike huwa na muonekano wa jinsia mbili, katika uke wake kwa juu au sehemu ambayo mwanamke hukeketwa, ile sehemu kwa fisi huwa na ukubwa mkubwa sana inaweza fika nchi saba, jambo hilo humfanya aonekane na muonekano wa jinsia mbili. Fisi wakikosana kwa kuibiana chakula au dume, na kwa bahati mbaya mmoja awe Mdogo, hupigana mpaka Mdogo kufa, na kama wapo sawa mnyonge hukimbia, wakati huo dume hubaki likishangaa tuu na kushindwa lianzie wapi
 
Usisubutu kumvizia fisi kwa nyuma, namna pekee ya kujirinda hurusha kinyesi chake kwa ghafla na atakuacha ukiwa umechanganyikiwa huku yeye akikimbia. Uoga kwake huisha akiwa na njaa Kali, kwa mfano hawezi kumuwinda binadamu mkubwa, lakini litokeapo suala la njaa Kali huwa hajali umri wa mtu. Watoto wake wanapofikisha umri wa miaka miwili mama yao huwatimua, wakajitegemee
 
Fisi anapokutana na watoto wa simba huwaua pasina huruma. Fisi dume halitakagi kusikia habari za watoto, huwa linaamini ni Mali ya jike, hivyo hanaga nao msaada kabisa. Fisi jike huwa na mwili mkubwa kuliko dume. Adui yao mkubwa ni mbwa mwitu, kwakuwa huwapora nyama ambazo wao wametafuta kwa tabu sana, pengine kwa kuhatarisha maisha yao. Fisi wanaogopa sana dume la simba, wanaweza kuwasumbua majike wa simba watatu lakini likija dume huwa linahakikisha mmoja kati yao anachechemea,
 
hivyo wanapomuona simba dume hupiga kelele za kupeana habari kuna hatari. Fisi ana uwezo mkubwa wa kunusa, hivyo ukifukia kitu hata chini anaweza kukitambua endapo tuu kina harufu ya damu damu. Viumbe hawa wakijihakikishia akiba ya chakula katika himaya zao, basi hufanya sherehe na sherehe zao huwa na ufanano na sherehe za binadamu, hucheza, hufurahi, hufanya ngono na ugomvi huzuka pia wakati huo watoto wote hufichwa ndani ya nyumba.
 
Fisi jike huweza kupiga dume mpaka likahama nyumba, na hutumia sana ujanja huu endapo jike linataka kuishi na mchepuko wake ndani. Fisi huamini pia katika umoja. ****************WANYAMA WABABE KWA FISI ***************** Fisi ni mnyama mnyonge sana na ni mnyama ambaye karibia wanyama wote wawindaji ni wababe kwake, kinachowasaidia ni hali ile ya kutembea makundi makundi yaani kifamilia, ndio huwafanya na wao waonekane kidogo wanajiweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…