Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mnyama huyu ni maarufu na pengine ndiye mnyama pekee mwenye kufahamika zaidi katika bara la Afrika, hususani hapa nyumbani, kwani mbali na kutokea katika hadithi, lakini pia mnyama huyu baadhi ya makabila humtumia wanapocheza ngoma za asili, pia ana sifa ya kuhusishwa sana na imani za kishirikina, baadhi ya jamii anapoonekana hupigwa mpaka kufa kwa imani kwamba ni mtu amejibadilisha kuwa fisi.
 
Jamaa hawa yaani fisi huishi kifamilia na kwa taarifa yako ni kwamba hujenga kabisa sehemu wanazokaa, urefu wao ni zaidi ya nchi 35, huwa na uzito wa kilo zaidi ya 75 inategemea na umri, huishi zaidi ya miaka 20, hubeba mimba kwa miezi mitatu na akizidisha ni siku chache sana,huzaa watoto kuanzia wawili mpaka wanne, kichwa chake hufanana na mbwa ila tofauti yao ipo katika muonekano
 
fisi ni mnyama ambaye miguu yake ya nyuma ni mifupi zaidi, hivyo unaweza ukamgundua kwa jinsi anavyotembea na matendo yake, huishi popote sehemu kame, vichakani na hata sehemu ambazo zina majani yenye ukijani sana, hivyo ni mnyama ambaye popote kwake ni kambi. Pamoja na kwamba ni mnyama ambaye jina lake linakuzwa sana kwamba anatabia ya kula mizoga,
 
lakini fisi ni mnyama anayewinda na hula nyama fresh, akikosa mawindo yake hufanya uporaji kwa wanyama kama simba na inapokosekana hata nafasi hiyo, basi akikutana na mfupa,mzoga yeye hana neno. Wakati wanyama wengine wengi wakiwa wanaongozwa na madume, ukifika katika koo za fisi majike ndio viongozi, lakini mbali na uongozi pia fisi jike ana nguvu za mwili kuliko dume,
 
bahati waliyonayo mbaya wanyama hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike lijifunguapo, watoto wao wengi hufa wakati mama yao anapozaa, hivyo kama jike atazaa wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.
 
b41a511828072b0ffb49fafc311a1f9e.jpg

Albadil imeanza kufanya kaz mtaan


Makubwa
 
bahati waliyonayo mbaya wanyama hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike lijifunguapo, watoto wao wengi hufa wakati mama yao anapozaa, hivyo kama jike atazaa wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.
 
SIFA ZAKE ZA KIPEKEE***************************** Mosi ni mnyama mnyonge lakini huweza kupola chakula kwa wanyama wakali kama simba. Fisi ni mnyama anayeweza kukimbia umbali mrefu kwa taratibu, we tangulia na spidi 120 yeye atakuja na 30 na atakukuta tuu njiani ukiwa umeanguka either kwa kuishiwa nguvu au misuli kukaza na hapo ndio atafanya biashara yake kwa urahisi, na sifa hii ndio watu husema eti anasubiri mtu adondoshe mkono wala sio kweli, ana akili zake.
 
Fisi huzaliwa akiwa macho ujue. Fisi jike huwa na maamuzi yote kuanzia mahabani mpaka mgawanyo wa kazi. Fisi dume ni mnyama bwege anatawaliwa na jike lake. Fisi ni kiumbe asiye na mbio za kasi. Fisi hunguruma, hucheka pia hutoa milio mbali mbali inategemea na alipo, na hiyo huwa ni lugha wanayotumia kuwasiliana akifanya hivyo wenzie wakisikia wanajua tuu kuna jambo gani limemsibu mwenzao.
 
Fisi jike huwa na muonekano wa jinsia mbili, katika uke wake kwa juu au sehemu ambayo mwanamke hukeketwa, ile sehemu kwa fisi huwa na ukubwa mkubwa sana inaweza fika nchi saba, jambo hilo humfanya aonekane na muonekano wa jinsia mbili. Fisi wakikosana kwa kuibiana chakula au dume, na kwa bahati mbaya mmoja awe Mdogo, hupigana mpaka Mdogo kufa, na kama wapo sawa mnyonge hukimbia, wakati huo dume hubaki likishangaa tuu na kushindwa lianzie wapi
 
Back
Top Bottom