Minde kwa mara yakwanza kabisa alipigwa picha mwaka 2003 na ilikuwa ni kutokana na kamera ambazo zilifungwa msituni katika suala zima la kufatilia maisha ya wanyamapori. Utaweza kuona ni hivi karibuni tu tangu mnyama huyu kugundulika vizuri na kwa ufasaha zaidi. Na hii imepelekea baadhi ya sifa zake kutofahamika zaidi hasa kwa upande wa kuzaliana japo kuna tafiti zilifanyika nakuona kwamba majira yao yakuzaliana hayana tofauti sana na wanyama jamii yao. Tutakapofika kwenye kuzaliana tutaona angalau kwa uchache kuhusu minde.