Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-09-22-22-41-54.png
 
Tumezoea kupika tambi na nyama ya kusaga au kuzichemsha zenyewe, leo nawaletea mapishi tofauti ya tambi.

Mahitaji

1. Tambi
2. Sausage
3. Karoti kubwa 1
4. Chumvi
5. Mafuta

Matayarisho

1. Bandika sufuria jikoni na maji kiasi na uweke chumvi kiasi.
2. Kata kata sausage zako vipande vidogo vidogo.
3. Kwangua karoti kisha katakata vipande vidogo vidogo vya nusu duara.
4. Maji yakichemka weka mafuta kisha weka tambi na funikia zichemke.
5. Zikianza kuiva weka sausage na karoti, acha viive pamoja.
6. Epua, chuja maji na andaa mezani tayari kwa kuliwa.

Enjoy!
 
1. Kuondoa unga wa ngano uliogandia kwenye mikono kwa haraka.

Chukua unga wa mahindi na usugue mikono kisha uioshe na maji, unga wa ngano uliogandia utaondika kwa urahisi kuliko kuosha na maji pekee. Mbinu hii ni mahususi hasa pale unapopata simu ya haraka au inapotokea dharura na mikono yote imejaa unga unaoukanda.
 
2. Kugundua kama magadi (baking soda) bado yanafaa au la

Inawezekana unayo magadi kwa muda mrefu na huna uhakika kama bado yana nguvu. Chukua vinega na weka kwenye kikombe, nusu kikombe, kisha weka kijiko cha chai kimoja cha magadi kwenye hiyo vinega, ikitoa gesi kama soda basi ujue magadi yako bado yana nguvu.
 
Back
Top Bottom