Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matunda ni mazuri sana kwa afya ya mlaji. Saladi ya matunda ni mlo kwa ajili ya watu wa rika zote na kwa wakati wowote. Ni muhimu zaidi kwa watoto, wagonjwa, wazee na wale wanaotaka kupunguza uzito. Unaweza kula saladi hii na maji, juisi halisi ya matunda au ‘smoothie’, hii ni juisi ya matunda isiyochujwa wala kuwekewa kitu chochote na ni nzuri sana kwa afya yako.
 
Mahitaji

Nanasi Nusu
Tikiti maji robo
Kipande cha papai
Embe moja
Apple moja
Tango nusu
Karoti moja
Maandalizi
1. Osha matunda yako vizuri na maji safi kisha toa maganda na uyaweke kwenye chombo kisafi.
2. Katakata matunda yako katika vipande vidogo vya mraba na kuweka kwenye bakuli safi, tumia bakuli maana ukiweka kwenye sahani unaweza poteza juisi za matunda hayo.
3. Changanya pamoja kisha weke kwenye friji ili ipate ubaridi kidogo.
4. Andaa mezani tayari kwa kuliwa.
NB: Ukipenda unaweza kukamulia nusu kipande cha limao.
Mlo huu unafaa sana kama ‘snack’ ya jioni wakati mnasubiri chakula cha usiku au kama dinner kwa wale wanaotaka kupunguza uzito.
 
Ni vyema ukawa na kawaida ya kuhifadhi vyakula vya aina mbalimbali nyumbani kwako ili ikusaidie pale unapotaka kupika. Haipendezi kila unapotaka kupika basi unaenda dukani au gengeni kununua kitu hicho. Kama una kipato cha uhakika kila mwezi ni vyema ukawa na hifadhi ya mwezi kwa vile visivyoharibika na ya wiki mbili na wiki wiki kwa vile vinavyoweza kuharibika upesi.
 
Hifadhi ya mwezi inaweza kuwa na vitu kama:

Mchele
Sukari
Unga wa Sembe
Unga wa Ngano
Maharage
Choroko
Mafuta ya Kupikia
Chumvi
Majani ya chai
Masala mbalimbali (samaki, pilau, kuku n.k.)
Nyanya za kopo
Tambi (Spaghetti)
Baking Powder
Hamira
Blueband, Jam, Mayonnise n.k
n.k
 
Hifadhi ya wiki mbili ni kama:

Njegere
Mayai
Vitunguu saum
Tangawizi
Vitunguu maji
n.k
Na sababu vingine huharibika mapema, unaweza kuwa unanunua kwa wiki wiki, mfano:

Nyanya
Viazi
Karoti
Pilipili hoho
Maziwa kama una freezer
Nyama ya ng’ombe, mbuzi, kuku n.k
Sausages
Samaki
n.k
Mboga za majani na matunda hivyo unanunua pale unapohitaji au kwa hifadhi ya siku 2-3 maana huharibika au kupoteza ladha upesi hata kama vikiwekwa kwenye friji.

Ha hivi pia ni vyema ukawanavyo ingawa sio vyakula, lakini inategemea na bajeti yako na uwezo wako.

Sabuni za kuoshea vyombo
Alluminium foil
Sponji za kuoshea vyombo
Toothpicks
Napkins
n.k
 
Screenshot_2017-09-22-23-04-00.png
 
Back
Top Bottom