Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. Unapotengeneza cup cake chache kuliko uwezo wa chombo chako cha kuoka

Kama unatengeneza cup cake 10 na chombo chako cha kuokea kinachukua cup cake 12, weka maji kwenye hizo nafasi 2 zinazobaki ili kuzuia kuungua kwa chombo chako cha kuokea.
 
c8eb39f234392191b3b08099803b041f.jpg
 
6. Kutafuta vipande vya glass vilivyovunjikia kwenye maji ya mapovu kwenye sinki ukiwa unaosha vyombo

Hii sijawahi kuitumia ila nasikia inafanya kazi, chukua bakuli pana la kioo (kama glass) na uweke juu ya maji na uitumie kama lensi kuangalia vipande vya glass vilivyo ndani ya maji.
 
Kuna tabia ambayo wamama wengi wanayo ya kuwa na vyombo vizuri vya gharama kubwa ambavyo hawavitumii kabisa katika matumizi yao ya kila siku na wanasubiri hadi wageni waje ndio vitumike. Anakuwa na seti nzuri za dinner na za tea, seti za vijiko na glass za kisasa lakini vinakuwa ni mapambo ya kabatini na wao wanatumia vyombo vya hali ya chini au vya plastiki kabisa. Watoto ndo kabisaa hawaruhusiwi kushika chombo cha udongo.
 
Mimi naona tabia hii sio nzuri, unaponunua vyombo inapasa iwe ni kwa ajili ya familia yako na mgeni akuja naye anakuwa sehemu ya familia. Sasa inakuwaje unamthamini mgeni anayekuja mara moja kwa mwaka kuliko watu unaoishi nao kila siku? Wakati mwingine inafika siku wageni wamekuja unatoa vyombo vipya hata wenyeji hawajui jinsi ya kuvitumia au unampa mtoto chombo cha kuvunika anatetemeka mikono sababu hajawahi kukitumia.
 
Wazoeshe watoto mapema kutumia vyombo ya udongo huku ukiwaekeza matunzo yake na jinsi gani vinavunjika. Hii pia ipo kwenye mashuka, vitaambaa vya makochi, vitambaa vya jikoni n.k. Nyumba ni yenu kama familia na sio ya wageni sasa kwa nini vitu vizuri viwe vya wageni na vibaya ndio vya familia?
 
Joto la Friji

Joto la friji halitakiwi kuwa zaidi ya nyuzijoto 5 za centigrade. Bakteria wanazaliana upesi ikiwa joto ni zaidi ya nyuzijoto 5 na ni hatari kwa vyakula vilivyohifadhiwa. Usiweke vyakula vya moto kwenye friji maana vitaongeza joto ndani ya friji.
 
Mahali pa Kuhifadhi

Kuna tofauti ya ubaridi kati ya ndani ya friji na kwenye mlango wa friji. Mlango wa friji unajoto zaidi hivyo usiweke vitu vinavyoharibika upesi kama maziwa au mayai. Vitu vinavyofaa kwenye mlango wa friji ni kama siagi, soda, jam n.k. Maziwa, mayai na vyakula vilivobaki baada ya mlo vihifadhiwe ndani ya friji kwenye shelfu. Matunda na mboga viwekwe kwenye container za friji ila njegere ili ziweze kukaa muda mrefu weka kwenye friza maana ukiweka kwenye shelfu zitaanza kutoa mizizi.
 
Usafi

Safisha uchafu mara tu unapomwagika na usiache hadi ukaukie hapo. Usiweke chakula hadi kikaharibika, kama ni chakula kimebaki kisikae zaidi ya siku nne. Angalau mara moja kwa mwezi uwe na siku ya kutoa vitu vyote kwenye friji na kuizima na kisha kusafisha kila sehemu. Zaidi kuhusu usafi wa friji soma Usafi wa jokofu kwenye link ya jikoni hapo kulia.
 
Back
Top Bottom