Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FIREFURY-hajjaj.jpg
 
1. Zima taa na vifaa visivyokuwa na uhitaji

Mara nyingi umeme mwingi hupotea kutokana na kuacha vifaa mbalimbali vikiwa vimewashwa bila sababu. Si jambo la kustajabisha watu kusahau taa za nje ya nyumba hadi saa sita mchana; au hata kuacha vifaa kama vile redio, televisheni au kompyuta vikiwa vimewashwa mchana au usiku kucha bila sababu ya msingi.
 
2. Tumia nishati mbadala

Kuna watu hufikiri kuwa kutumia nishati kama vile umeme kupikia ndiyo kuwa wa kisasa zaidi; lakini ukweli ni kuwa huku ni kujiongezea gharama zisizokuwa na sababu. Matumizi ya gesi na umeme jua (solar) ni nafuu zaidi kuliko kutumia umeme kwa kila kitu.
 
3. Ondoa vifaa vya zamani

Sera za dunia zimebadilika katika jitihada za kutunza mazingira. Vifaa vinavyozalishwa hivi leo, vingi hutengenezwa kwa kuzingatia kulinda mazingira kwa kuokoa matumizi ya nishati. Hivyo ni vyema ukaondoa vifaa vya zamani kama vile televisheni, kompyuta za mezani, redio, taa au jokofu ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya zamani inayotumia umeme mwingi. Mara ununuapo vifaa angalia vifaa vyenye nembo ya Energy Star ili kubaini vifaa ambavyo vimetengenezwa kwa kuzingatia kuokoa nishati.
 
Back
Top Bottom