Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4. Zima au punguza matumizi ya jokofu

Jokofu ni moja kati ya vifaa vinavyotumia kiwango kikubwa cha umeme. Kupunguza matumizi ya jokofu ina maana kuwa ni kubadili kiwango cha matumizi ya umeme. Unaweza kuwasha jokofu kwa muda fulani tu na si kwa siku nzima; pia unaweza kuepuka kufungua jokofu mara kwa mara ili kutunza ubaridi ndani ya jokofu ili lisiwashwe mara kwa mara.
 
5. Tumia pasi vizuri

Ni vizuri kupasi kila nguo unayoivaa, lakini matokeo yake kwenye matumizi ya nishati siyo mazuri. Watu wengi hawafahamu kuwa umeme mwingi sana hupotea wakati wa kupasi na kuwasababishia kulipa bili kubwa za umeme. Hata hivyo, yapo mambo unayoweza kufanya ili kuokoa matumizi ya umeme kwa kutumia vizuri pasi ya umeme.
 
Nunua pasi nzuri yenye viwango na ubora stahiki.
Nunua nguo zisizohitaji kupasiwa kila mara au kupasiwa kabisa.
Pasi nguo kwa pamoja. Ni vyema kupasi nguo tano kwa wakati mmoja kuliko kupasi kila siku nguo moja, kwani utapoteza umeme mwingi kupasha pasi moto mara kwa mara kila siku.
 
6. Tumia taa zinazookoa nishati

Hivi leo sokoni kuna aina mbalimbali za taa za umeme, lakini siyo zote zinafaa kwa matumizi yako. Balbu za zamani hutumia umeme mwingi zaidi huku zikikupa matokeo duni. Leo zipo taa zinazojulikana kama “Energy Severs” ambazo zimetengenezwa kwa kutumia teknolojia inayookoa nishati huku zikikupa matokeo mazuri zaidi.
 
7. Kagua mfumo wako wa umeme

Mfumo duni wa umeme (wiring) kwenye nyumba yako unaweza kusababisha upotevu mkubwa wa umeme. Kwa mfano ikiwa umeme unavuja kimakosa na kuingia kwenye waya wa aridhini (earth), umeme mwingi utapotea kwenda kwenye ardhi bila wewe kujua. Unaweza kumtafuta fundi au mtaalamu wa masuala ya umeme wa nyumba, ili aweze kukusaidia kukagua mfumo wako na kuhakikisha kuwa hakuna sehemu inayovujisha na kukupotezea umeme.
 
8. Tumia feni na kiyoyozi vyema

Mara nyingine kutokana na mazingira ya joto mtu anahitaji kutumia feni (pangaboi) au kiyoyozi ili kukabili joto. Ni vyema ukafahamu kuwa vifaa hivi huhitaji umeme ili kujiendesha; hasa kiyoyozi huhitaji umeme mwingi ili kufanya kazi. Pamoja na hilo, ni dhahiri kuwa yapo mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kuokoa umeme unaotumiwa na kiyoyozi na feni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…