Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-09-29-11-06-31.png
 
4. Ni kwa namna gani unailisha akili yako chakula?
Unatakiwa kuilisha chakula akili yako na chakula cha akili au ubongo wako ni maarifa na siyo kitu kingine. Jiulize katika taaluma uliyosomea umeshasoma vitabu vingapi vya kuongeza maarifa tofauti tofauti na vitabu vya darasani yaani ambavyo haviko katika mtaala wa darasani? Tokea umalize shule au chuo ni mara ngapi umesoma kitabu kwa ajili ya kuona akili yako?
Hapa ndipo tunapwaya sana sisi. Hata sasa hapa nipo library. Kuna vizee hapa vizungu vinajisomea na vingine vimejaza makapu ya vitabu vinaazima vikajisomee nyumbani. Ndiyo maana imesemwa kwamba ukitaka kumficha kitu Mwafrika basi kiweke kwenye vitabu!
 
Mwisho, somo letu la leo lilitualika kuweza kujiuliza maswali muhimu katika maisha yetu ili tuweze kupata matokeo tofauti. Ili tubadilishe maisha yetu ni lazima kwanza tubadilishe namna ya kufikiri kwanza na njia nzuri ya kufikiri ni pamoja na kujiuliza maswali muhimu na makini kwenye maisha yako. Nakutakia utekelezaji mwema katika haya uliyoweza kujifunza leo.
Asante daktari. Leo umeleta mambo ya muhimu sana. Umenikumbusha mambo mengi. Nimeamka !!!
 
Back
Top Bottom