Asante sana mkuu. Hata mimi nilikuwa kama wewe. Mtu alikuwa akinitukana humu nilikuwa naumia sana. Baada ya kusoma soma vitabu mbalimbali vya kisaikolojia ndiyo nikajifunza mbinu hizi na zimeniokoa na mambo mengi pamoja na maugomvi mengi yasiyo na kichwa wala miguu. Mpaka imefikia sasa nikitaka kupima afya ya kisaikolojia ya watu naenda kule Jukwaa la Siasa na kuchangia hoja nzuri tu, naporomoshewa matusi wee halafu narudi huku kwenye uzi wetu huu wa upendo. Ni kitu cha kawaida; na silaha pekee inayoweza kuushinda uovu, majeraha na mizigo mizito waliyobeba watukanaji hawa ni upendo. Hakuna kitu kinachouma kama mtu anakuporomoshea matusi na anategemea kuwa nawe utajibu matusi ili bifu liendelee ikibidi mpaka upigwe ban na badala yake unamjibu (si kwa unyonge wala kujidharaulisha), "Asante mkuu. Mungu Anakupenda. Nitakuombea" halafu unaachana naye.
Binafsi ningependa uendelee kubakia katika uzi huu. Uzi huu unaweza kuuona kuwa ni wa kipuuzi lakini baadaye utagundua kuwa karibu vionjo vyote vya JF vimo humu: Michezo, mapenzi, elimu, afya, utani n.k. Na faida kubwa ni kwamba huku matusi kidogo tunajaribu sana kupambana nayo; na watukanaji wakija huku wanatukana wee, tunawapuuza na mwisho wanakwenda zao. Naamini kilichotokea leo ni bahati mbaya tu lakini kusema kweli huku tunaishi kwa amani sana. Karibu sana !!!